Aliyekuwa Katibu na Msemaji wa Chama cha Madereva, Rashid Saleh amefariki dunia ghafla huku chanzo cha kifo chake kikizua utata miongoni mwa wananchama wa chama hicho na wananchi.
Taarifa za awali kifo cha Rashid Swaleh zilielza kuwa alifariki baada ya kuugua ghafla ugonjwa ambao bado haujabainika.
Madereva
na wananchi wengine walifika katika hospitali ya Muhimbili wakiwa na
majonzi makubwa huku wakisubiri mwili huo wa marehemu upimwe ili kubaini
chanzo cha kifo chake.
Baadhi ya madereva waliozungumza na
waandishi wa habari walieleza kusikitishwa na msiba huo wa ghafla na
kueleza kuwa huenda msemaji wao aliyekuwa anapigania kwa nguvu zote haki
zao amenyamazishwa.
“Sisi kama madereva hatutakubali, kama kosa
lake yeye ni kutetea haki za watu, hili ni tatizo,” alisema mmoja wa
madereva hao aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Mdem.
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alifika katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili na kuwataka madereva hao kutokata tama bali
waendelee kudai haki zao huku wakisubiri majibu ya madaktari kubaini
chanzo cha kifo cha msemaji wao.
“Hii isiwakatishe tamaa kuendelea
kudai haki zenu ambazo ni za msingi kutoka kwa ajili wenu,” alisema
huku akiwasihi kutofifishwa moyo katika kutafuta haki zao za msingi.
No comments:
Post a Comment