Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NIC, Hamida Simbaulanga akikabidhiana cheki ya shilingi 5,500,000 na Afisa
utawala wa hospitali ya Medewell, Amina Ramadhani, baada ya wafanyakazi
wa benki ya NIC kutembelea Hospitali ya Medewell iliyopo Kibaha Mkoani
Pwani.
Afisa
utawala wa hospitali ya Medewell, Amina Ramadhani akitoa maelekezo kwa
viongozi wa benki ya NIC mara baada ya wafanyakazi wa benki ya NIC
kutembelea katika hospitali hiyo mwishoni mwa wiki Kibaha Mkoani Pwani.
Baadhi
ya wagonjwa waliofika kupatiwa matibabu ya Mtoto wa jicho katika
Hospitali ya Medewell iliyopo Kibaha Mkoani pwani. Na sehemu ya jicho
iliyobandikwa kilebo ndilo jicho lenye tatizo la Mtoto wa jicho ndilo
litakalo fanyiwa upasuaji katika hospitali hiyo.
Wagonjwa wenye tatizo la Mtato wa jicho wakiwa katika foleni ya kuingia kwa Daktali.
BENKI
ya NIC imeipiga jeki hospitali ya Medewell inayohudimia wagonjwa wa
matatizo ya mtoto wa jicho bila gharama yoyote iliyopo kibaha Mkoani
Pwani kiasi cha shilingi 5,500,000 ili kuweza kuhudumia wangonjwa kwa
ufasaha zaidi na kupata matokeo mazuri kwa jamii inayopatwa na maradhi
hayo. Ikiwa Ugonjwa wa Mtoto wa jicho huwapata zaidi wazee kwa kupoteza
nguvu ya jicho kuona kwa ufasaha.
Benki
hiyo imetoa msaada huo kwa wagongwa 25 wanaosubiri kufanjiwa upasuaji
pamoja na hospitali hiyo kuwa na wagonjwa 37 wenye matatizo ya hayo
ikiwa kila mgonjwa anaghalimi dola za Kimarekani 100.
Akizungumza
katika makabidhiano ya msaada huo Mkurugenzi mkuu wa Benki ya NIC,
Pankaj Kansara amesema kuwa benki hiyo imetoa msaada huo kwa kuwa
wameona hospitali ya Medewell imejitolea kutoa huduma ya upasuaji wa
wagonjwa wenye tatizo la mtoto wa jicho kutokana na hospitali hiyo kutoa
huduma hiyo bila gharama yoyote.
Kwa
upande wa wagonjwa wanaosubiri kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya
Medewell walishukuru madaktari wanaotoa huduma katika hospitali hiyo
kuwa wanatoa huduma kwa upendo na kuwafariji pia ikiwa wakiwepo
huspitali hapo wanapewa chakula na marazi bila kutoa huduma yoyote.
Ilibainika
kuwa wagonjwa hao wanaosumbuliwa na tatizo la mtoto wa jicho ni kutoka
sehemu tofauti tofauti hapa nchini, ikiwa ni Mwanza, Mheza, Tanga,
Kilimanjaro na Kilwa.
Nae
Afisa utawala wa hospitali ya Medewell, Amina Ramadhani amewashukuru
wafanyakazi wa benki ya NIC kwa kuona mahitaji ya jamii inayopatwa na
matatizo ya Mtoto wa jicho.
Wafanyakazi
wa Benki ya NIC wakipima kisukali katika hospitali ya Medewell iliyopo
Kibaha Mkoani Pwani mara baada ya kutembelea hospitali hiyo.
Viongozi wa benki ya NIC wakimsikiliza mkurugenzi wa Mradi wa hospitali ya Medewell, Shiraz Datoo.
Wafanyakazi
wa Benki ya NIC wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
Hospitali ya Medewell mara baada ya kukabidhiana cheki ya shilingi
5,500,000.
Viongozi wa beni ya NIC wakiagana na kiongozi wa Hospitali ya Medewell.
No comments:
Post a Comment