Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo
akikata utepe kuzindua Kisima cha maji safi na salama katika kijiji cha
Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma mwishoni mwa juma lililopita.
KIJIJI
cha Manchali kilichopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, kimekabidhiwa
mradi wa dola za Marekani 150,000 wenye lengo la kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi
huo ulikabidhiwa kijiji hicho na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa
mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez.
Mradi huo umelenga kusaidia jamii inayoishi katika kijiji hicho kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi
huo wa nishati ya jua umelenga kutatrua tatizo la nishati na kufanya
matumizi bora ya ardhi na teknolojia ya maji.Mradi huo unasaidia familia
600.
Kwa
uzoefu wa Tanzania na maeneo mengine duniani, familia maskini ndizo
zinazopigika vibaya na mabadiliko hayo na ndio haizna uwezo wa
kukabiliana nayo.
Kwa mradi huo wananchi wa Manchali wanatarajia kukabiliana vilivyo na mabadiliko ya Tabia nchi.
Akizungumza
katika kijiji hicho cha Manchali, Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Bi. Awa
Dabo alisema kwamba ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
uwezeshaji wananchi kiuchumi ni muhimu sana ili kufanya familia kustawi.
Kisima kilichozinduliwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo.
“Athari
za mabadiliko ya tabia nchi kwa watu maskini ni kubwa na ndio
wanaoathirika zaidi” alisema Mkurugenzi Mkazi UNDP Bi. Dabo.
Aidha
alisema kwamba anaishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea
kuhangaikia suluhu ya watu kukubali kuwapo kwa mabadiliko ya tabia nchi
na kufanya juhudi ya kukabili hali hiyo.
“Hii
imo katika malengo ya maendeleo endelevu kwani malengo manne kati ya 17
yanahusiana na mabadiliko ya tabia nchi na kuhifadhi mazingira.kwa
kutumia fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo, UNDP imefanikiwa kusaidia
wananchi wa kijiji cha Manchali kufanyia kazi maeneo kadha muhimu ili
kufanya uragibishi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, kuongeza kasi ya
upoandaji wa miti na matumizi ya nishati jadidifu.” alisema.
Bi Dabo amesema kwamba mradi huo wa Manchali umekamilika ni mmoja wa mradi yenye mafanikio inayosimamiwa na UNDP.
Aliwapongeza
wananchi wa Manchali kwa ushiriki wao na kuufanya mradi huo kuwa
wakwao hali iliyosababisha kuwepo na matunda yenye tija katika kijiji
hicho.
“Sisi UNDP kutokana na mafanikio haya tunaangalia maeneo mengine ya kufanya mradi kama huu” alisema Bi Dabo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
akizindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi
kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in
vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino
District), kijijini humo.
Naye
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro
Rodriguez alisisitiza ushiriki wa wananchi katika kufaniukisha miradi na
kusema kwamba mradi huo umefanikiwa kutoka na ushiriki wa wananchi na
hasa kitendo chao cha kuufanya mradi huo kuwa mali yao.
Aliongeza
kwamba kitendo cha kufanya mradi wao na kuwa viongozi wa maendeleo yao
wao wenyewe kumefanya mradi uwe na tija kubwa kwao.
“Mradi
huu umeleta maendeleo makubwa kwa wananchi wa hapa kutokana na wao
kuanza kutumia nishati jadidifu, watoto wanakwenda shule na maeneo
yameanza kurejewa na misitu.”
Mratibu
huyo aliongeza kwamba mabadiliko ya tabia nchi ni ya kweli na wala si
ya kuyafanyia mzaha, mashirika ya umoja wa mataifa na Umoja wenyewe
wanatazama sana athari zake mbaya.
Alisema
kijiji cha Manchali kimefanikiwa katika kuanza kukabili mabadiliko ya
tabianchi kwa kubadili mambo yanayowazunguka na kurejesha uoto wa asili
na kuacha kuharibu mazingira huku shughuli za maendeleo zikichukua sura
mpya yenye kujali mabadiliko ya tabia nchi.
Bango la mradi uliozinduliwa na Bw. Alvaro Rodriguez.
Kutoka
kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum,
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa
Dabo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez katika picha ya pamoja na viongozi wa kijiji wakiwakilisha
wananchi ambao watanufaika na mradi huo.
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP), Awa Dabo, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP),
Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk.
Hashina Begum katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment