Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema ongezeko la wapigakura limetokana na idadi hiyo kuongezeka baada ya kufanya uhakiki kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura kabla ya Uchaguzi Mkuu.
Kabla
ya uchaguzi huo uliofanyika Jumapili iliyopita, katika taarifa yake,
tume ilisema jumla ya wapiga kura 23.78 milioni waliandikishwa katika
Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa Biometric Voters
Registration (BVR).
Baadaye
tume hiyo ilipochambua taarifa za daftari hilo ilibaini kasoro na
kuondoa wapiga kura zaidi ya milioni moja na kubaki na wapiga kura 22.75
milioni.
Daftari
hilo lilibaki NEC huku vyama vya siasa vikipewa nakala za daftari kwa
ajili ya kumbukumbu zao. Hata hivyo, maswali yaliibuka siku NEC
ilipotangaza matokeo ya urais baada ya Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu
Damian Lubuva kusema watu waliojiandikisha kupiga kura idadi yao ni 23
milioni, idadi ambayo ni sawa na ile ya awali kabla ya wale milioni moja
kuondolewa.Kati ya hao, waliopiga kura walikuwa 15,589,639.
Utata
huo umeshalalamikiwa na baadhi ya vyama vya upizani vikiwamo vile
vinavyounda Ukawa ambavyo viliitaka NEC kutoa ufafanuzi.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari NEC, Clarence Nanyaro jana alizungumzia suala hilo na kusema ongezeko hilo limekuja baada ya kupeleka daftari kwenye vituo walikojiandikisha watu kwa ajili ya uhakiki.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari NEC, Clarence Nanyaro jana alizungumzia suala hilo na kusema ongezeko hilo limekuja baada ya kupeleka daftari kwenye vituo walikojiandikisha watu kwa ajili ya uhakiki.
Alisema
kuna watu waliojiandikisha na walipokwenda kuhakiki majina yao kwenye
vituo walivyojiandikisha, hayakuonekana kwenye takwimu za tume.
“Tulifanya uhakiki siku za mwisho karibu na uchaguzi na kubaini kulikuwa na watu wengi ambao majina yao yalikuwa hayaonekani,” alisema Nanyaro
Alisema kutokana muda kuwa mdogo, hawakuweza kutoa nakala nyingine kwa vyama vya siasa kama walivyofanya awali.
No comments:
Post a Comment