Katibu
mkuu wa TEWUTA, Junus Ndaro (katikati) alkizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mwenyekiti wa TEWUTA, Pius Makuke, kushoto ni afisa kutoka chama hicho.
Na Rabi Hume
[DAR ES SALAAM] Chama
cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania
(TEWUTA), kimemtaka rais wa Tanzania, Dr. John Magufuli kuyasaidia
mashirika ya mawasiliano yaliyo chini ya seikali kutokana na mashirika
hayo kuwa na hali mbaya ya utoaji huduma na mfumo mzima wa manejimenti
zake.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo, Katibu Mkuu wa
Tewuta, Junus Ndaro alisema mashirika ya mawasiliano yaliyochini ya
serikali ya Posta na TTCL yamekuwa yakizidi kuwa na hali mbaya na mtu
pekee anayeweza kuyaokoa ni rais.
Ndaro
amesema kuwa mashirika yaliyochini ya serikali ya Posta na TTCL
yamekuwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikichochewa na viongozi
wanaoongoza mashirika hayo na kuhitaji rais kuingilia jambo hilo ili
kuyasaidia mashirika hayo yarudi kama awali.
“Sisi
kama TEWUTA tunamtaka rais Magufuli kwa kutumia kauli yake ya hapa kazi
tu basi na hizi sekta za mawasiliano aweze kuyasaidia mashirika hayo
ambayo kwa sasa yapo katika hali mbaya,” alisema Ndaro.
Katibu
Mkuu huyo ametolea mfano Shirika la Simu Tanzania (TTCL) kuwa limekuwa
na utendaji mbovu wa kazi na kuwatupia lawama viongozi wa shirika hilo
kwa kuwa na tabia ya kujilipa mishahara mara mbili kwa mwezi na kupeana
fedha ya nauli kila mwezi 600,000 huku wafanyakazi wa kawaida wakiwapa
42,000 pekee.
Aidha
kupitia mkutano huo na waandishi wa habari, Ndaro ametumia fulsa hiyo
kuzungumza kwa niaba ya TEWUTA aina ya Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia ambae wanadhani atakuwa mtu sahihi kutatua matatizo ambayo
yatakuwa yanatokea ndani ya sekta hiyo kuwa anatakiwa kuwa mzalendo kwa
kufanya kazi kwa kujua kwamba anasaidia nchi yake.
Sifa
nyingine ambayo amesema waziri huyo anapaswa kuwa nayo ni kuwa mchapa
kazi na kuwa tayari kufanya kazi muda wowote ambao atahitajika kufanya
kazi na asiwe anamiliki hisa katika shirika lolote la mawasiliano kwa
sababu akiwa mtu ambaye ana hisa atapendelea mashirika yasiyo ya
serikali.
“Chama
cha Wafanyakazi cha TEWUTA tunawasilisha ombi rasmi kwake, kuwa iwapo
ataunda Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa faida ya sekta
ya mawasiliano tunaomba achague kiongozi ambaye ni mzalendo na
mchapakazi ili aje kufanya kazi ya kutatuua changamoto hizi,
“Sifa
nyingine lazima asiwe na hisa katika kampuni yeyote ya mawasiliano,
tukiwa na kiongozi mwenye hisa kwenye makampuni mengine hatakuwa
akiyasimamia vyema mashirika ya serikali badala yake ataangalia makapuni
binfasi,” alisema Ndaro.
Pamoja
na hayo pia wametoa mapendekezo yake kwa rais ambayo ni pamoja na
kuteua wajumbe wapya wa bodi ya wakurugenzi wakiamini kuwa wajumbe hao
ndiyo wamekuwa wakishinikiza shirika hilo kuwa kufanya mambo ambayo ni
kinyume na taratibu licha ya kuwa na Mwenyekiti mpya Bw. Tolly Mbwete
ambaye hawezi kufanya maamuzi pekee bila wajumbe kuridhia.
Pendekezo
lingine ambalo wamelitoa kwa rais Magufuli ni kuifukuza kampuni ya
RubieM ambayo kwa mujibu wa TTCL ilikuja Tanzania mwaka 2013 kwa mkataba
wa miezi sita (6) kwa ajili ya kuwa wanatoa ushauri kwa shirika jinsi
ya kufanya biashara kisasa lakini wamekuwa wakifanya kazi hadi sasa na
kwa maelezo ya Tewuta wamefanya uchunguzi na kugundua kampuni hiyo ina
kashfa nyingi za ufisadi na kuamini yawezekana kuna ufisadi unaofanyika
kwenye shirika la TTCL.
Mambo
mengine ya kawaida ambayo wamemuomba rais ni pamoja na kupunguza kodi
kwa wafanyakazi, kuitaka TTCL kupunguza tozo ya kuunganisha simu
(interconnection cherge) ili kuwapatia unafuu wananchi wa kawaida kuweza
kufurahia huduma kutoka kwa shirika la simu.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Taifa wa TEWUTA, Pius Makuke amesema wamefikia
hatua ya kuweka wazi mambo hayo kutokana na mambo kuzidi kuwa mabaya na
walizungumza na uongozi wa TTCL lakini hakuna hatua waliyochukua na sasa
wanafata kwa rais kama na yeye hatochukua hatua yeyote basi watakwenda
mahakamani.
No comments:
Post a Comment