Kaimu Mkurugenzi jiji la Mbeya Dkt, Samuel Razalo.
Na Emanuel Madafa, Mbeya
HALMASHAURI
ya Jiji la Mbeya, imesema imejipanga vyema katika kuhakikisha mradi
mkubwa wa soko jipya la mwanjelwa unasimamiwa kikamilifu kwa kufuata
taratibu za serikali sanjali na mikataba iliyoingia na benki ya CRDB
kwa kipindi cha miaka 15.
Mradi
huo wa soko la kimataifa la Mwanjelwa lililopo jijini Mbeya ujenzi
wake imefikia asilimia 99 hivyo upo katika hatua za mwisho za
kukamilika kwake.
Akizungumza
ofisini kwake, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dkt. Samweli Razalo,
amesema licha ya soko hilo kukamilika lakini mchakato wake wa uendeshaji
utazingatia taratibu za halmashauri na mkataba walioingia na benki ya
CRDB.
Amesema
hatua hiyo, inatokana na halmashauri ya Jiji hilo kukopa kiasi cha
shilingi Bilioni 13 kutoka benki ya CRDB na kufanikisha ujenzi wa soko
hilo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 10 tangu lilipoteketea kwa moto.
Muonekano wa Mradi wa Soko la Mwanjelwa Jijini Mbeya ambapo ujenzi wake bado unaendelea.
Amesema,
benki hiyo kwa kukubaliana na halmashauri imepanga kiasi cha kodi
kitakachopaswa kulipwa na wafanyabiashara kuanzia shilingi elfu moja
kwa siku hadi shilingi 500,000 kwa mwezi.
Amesema
Wafanyabiashara ambao watatumia meza watatakiwa kulipa ushuru wa
shilingi 1000 kwa siku huku wale wa maduka watalipa kiasi cha shilingi
500,000 kwa mwezi na wauza nyama watapaswa kulipa kiasi cha shilingi
400,000 kwa mwezi,”alisema.
Amesema
, awali halmashauri hiyo ilipokea maombi kutoka kwa wafanyabiashara
ambao walikuwa wakiomba kupunguzwa kwa gharama za tozo hizo kwani ziko
juu ukilinganisha na hali ya uhumi wa sasa.
Amesema,
halmashauri iliyachukua maombi hayo na kuyawasilisha kwenye mamlaka
husika ya benki ya CRDB hivyo wanasubili majibu na kuwataka
wafanyabiasha kuwa wapole wakati wanasubili majibu hayo kutoka kwenye
uongozi wa benki hiyo.
Soko
la Mwanjelwa liliteketea kwa moto mwaka 2006 na kusababisha hasara ya
mamilioni ya fedha kutoka kwa wafanyabiashara zaidi ya 2000 walionguliwa
maduka yao na ujenzi wake kuanza mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment