Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza idadi ya madiwani wa viti maalumu pamoja na vyama wanavyotokea.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima
ametaja idadi ya madiwani hao kuwa 1402 na kuwataja madiwani 1392 huku
15 wakisubiri chaguzi zimalizike katika kata zilizosalia.
Amesema katika madiwani hao CCM ni 1122, Chadema 220, CUF 49, NCCR 6 na ACT 6.
Kailima
ameongeza kuwa kata ambazo bado hazijafanya uchaguzi ni kata 34 ambapo
kupitia kata hizo wanatarajia kupata madiwani wa viti maalum 15.
Amesema
halmshauri ambazo bado hazijakamilisha uchaguzi zitasubiri uchaguzi
ukamilike kwa kata zote ndiyo waunde baraza la halmashauri na kazi ya
kwanza kwa baraza hilo ni kuchagua meya wa halmashauri husika.
No comments:
Post a Comment