Mkurugenzi wa huduma kwa wateja
wa Artel Bi. Adriana Lyamba akimuhudumia Bw. Ally Janja ambae ni Meneja
wa Tawi la NBC Kilimanjaro na pia mmmoja kati ya wateja maalum wa Airtel
wakiwa katika dula jipya la Airtel Moshi lenye kona maalum kwa wateja
hao (Airtel Premium) mara baada ya duka hilo jipya na lakisasa
kufunguliwa jana na Airtel mkoani Kilimanjaro.
Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma
kwa wateja Bi. Adriana Lyamba akijadiliana jambo na Meneja wa tawi la
Biashara la Airtel Mkoa Kilimanjaro, Bw. Paschal Bikomagu (kushoto) na
msimamizi wa maduka hayo bw, Thomas Chalamila mara baada ya Airtel
kuzindua…
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja
wa Artel Bi. Adriana Lyamba akimuhudumia Bw. Ally Janja ambae ni Meneja
wa Tawi la NBC Kilimanjaro na pia mmmoja kati ya wateja maalum wa Airtel
wakiwa katika dula jipya la Airtel Moshi lenye kona maalum kwa wateja
hao (Airtel Premium) mara baada ya duka hilo jipya na lakisasa
kufunguliwa jana na Airtel mkoani Kilimanjaro.
Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma
kwa wateja Bi. Adriana Lyamba akijadiliana jambo na Meneja wa tawi la
Biashara la Airtel Mkoa Kilimanjaro, Bw. Paschal Bikomagu (kushoto) na
msimamizi wa maduka hayo bw, Thomas Chalamila mara baada ya Airtel
kuzindua duka la kisasa moshi mtaa wa mandela jana au soko kuu.
Toka
kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Kaskazini (TCRA)
Eng. Annette Mahimbo Matindi na Afisa Tarafa wa Moshi Mashariki bi
Evelyne Zakaria (kati) wakiwa na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa
Airtel Bi. Adriana Lyamba wakishirikiana kukata utepe wakati Airtel
ikizindua duka jipya mkoani Kilimanjaro mtaa wa Mandela jana. Kulia
wakwanzani akishudia ni Meneja wa Biashara wa Airtel Kanda ya Kaskazini
Bw. Brighton Majwala.
Picha ya pamoja
• Wateja kufurahia uwepo wa huduma bora na za kisasa.
KAMPUNI ya mawasiliano
ya simu za mkononi Airtel leo imefungua duka jipya na la kisasa mjini
Moshi lililopo katika mtaa wa Soko Kuu. Uzinduzi wa duka hili
linadhihirisha ahadi yake kwa Airtel kujali wateja wake Tanzania nzima
na kuwapa huduma iliyobora na ya kiwango cha juu popote pale walipo.
Hii ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo
kuhakikisha wanatoa na kuboresha mpango wake wa huduma kwa wateja wake
ili kuongeza urahisi wa kuwafikia wateja wake mbalimbali popote pale
walipo nchi nzima.
Akizungumza katika sherehe fupi ya
ufunguzi wa duka hilo,mkurugenzi wa kitengo cha huduma za wateja wa
Airtel, Bi Adriana Lyamba, alisema kuwa ufunguzi wa duka hili jipya na
la kisasa mjini Moshi ni mwendelezo wa malengo ya Airtel kuendeleza
kuboresha maisha morani kwa kila mtanzania kwa kupata huduma zenye zenye
ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote walipo.
"Tunafuraha kubwa sana kuona
tunafanikiwa kuwafikia wateja wetu na kufungua milango kwa wateja zaidi
mjini Moshi na kuwahakikishia kuwa tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa
kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi
ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama
haya kwa ajili ya kuwasogezea huduma karibu na wananchi, na
ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia , "alisema
Lyamba
Duka hili jipya lenye mazingira mazuri
kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Airtel
ikiwemo huduma za modem, Airtel Money, simu mpya za kisasa za
smartphone, huduma zetu za intanet na huduma ya malipo ya bili za awali
na mwezi .
Bi, Evelyne Zakaria ambae ni Afisa
tarafa wa Moshi Mashariki kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus
Makunga aliwashukuru Airtel kwa dhamira yake ya uboreshaji wa huduma kwa
wakazi wa mji wa Moshi. Pia alibainisha kuwa mawasiliano ni jukumu
kubwa katika kuunganisha watu na biashara ya kuendesha maendeleo katika
Kata ya Moshi.
Mkuu wa Wilaya aliyaomba makampuni
mengine ya simu yajitokeze zaidi na kuiga mfano wa Airtel katika kutoa
huduma bora kwa wakazi wa mji wa Moshi akisema kuwa ofisi yake iko
tayari kwa kutoa ushirikiano kwa lengo la kufanya maisha bora kwa wakazi
wake.
No comments:
Post a Comment