Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge (mbele walioingia mtaroni)
na watumishi wengine wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakishiriki zoezi la
kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Roadmapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge (katikati aliyeshika
koleo) akiongea kuhamasisha zoezi la watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa
kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo
Wafanyakazi
wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Tume ya Maendeleo ya Ushirika
wakijiorodhesha baada ya kumaliza zoezi la usafi wa mazingira mapema
leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais
la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira, orodha
hiyo itatumika kuwabaini watumishi ambao hawajashiriki zoezi la usafi.
Wafanyakazi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
Wafanyakazi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Dodoma Bazil Mwiserya akishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
Watumishi wa Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kufanya usafi kwa kufyeka magugu eneo la makaburi ya Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge (katikati aliyeshika
koleo) akiongoza zoezi la watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa kusafisha
mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo
Wafanyakazi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
Mkoa wa Dodoma umeanza rasmi
kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli lililotaka kufanyika kwa usafi wa mazingira katika maeneo
mbalimbali ya nchi siku ya tarehe 9 Disemba, 2015 kama mojawapo ya maadhimisho
ya siku ya uhuru na kuwataka viongozi na wataalamu kusimamia utekelezaji wa
agizo hilo.
Uongozi wa Mkoa umeamua kuanza
mapema zoezi la ufanyaji usafi pasipo kusubiri tarehe 9 Disemba na umepanga
kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu likihusisha usafi wa kila siku na usafi wa
siku zote za Jumamosi kuanzia saa 1:00 hadi saa 3:00 asubuhi.
Taasisi mbalimbali zilizopo
Mkoani Dodoma zimetumia Jumamosi ya leo Novemba 28, 2015 kushirikiana na
wananchi kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma ambapo
Viongozi na Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ofisi ya Tume ya
Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wamefanya usafi eneo la Bahi Road
kuelekea Nkuhungu kwa kuondoa taka na michanga kwenye mitaro ya maji ya mvua,
kufyeka na kuchoma taka eneo la makaburi ya Kizota.
Kwa mujibu wa Ratiba ya usafi
iliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Mamlaka ya majisafi na usafi
wa Mazingira mjini Dodoma-DUWASA ilifanya usafi eneo la kuanzia ofisi za waziri
mkuu (Mtaa wa Mahakamani) hadi ofisi za
hazina ndogo.
TANESCO Mkoa wa Dodoma
walisafisha eneo la kituo cha kuuzia mafuta cha BP Capital hadi soko la
Sabasaba. Taasisi nyingine ni pamoja na jeshi la Magereza ambapo lilifanya
usafi kuanzia mzunguko wa barabara ya kuelekea Bahi hadi maeneo ya magorofa
mengi wakati mabenki yalisafisha mitaa na barabara zinazopita mbele ya majengo
yao ya benki na Wakala wa Barabara TANROADS wao walisafisha kuanzia kituo cha
mabasi ya mikoani hadi soko la Sarafina.
Kwa upande wa wananchi
walioshiriki zoezi hilo la kufanya usafi, wamepongeza utaratibu na kusema
utasaidia kuweka mji katika mazingira safi. Akiwawakilisha wananchi
walioshiriki zoezi hilo, Mkazi wa Dodoma Onesmo Stephano alielezea kuwa
utaratibu huo wa viongozi wa Mkoa na watumishi wa serikali kushiriki kufanya
usafi unawatia hamasa kubwa wananchi nao kushiriki pale wanapoona viongozi wao
wanashiriki kufanya nao usafi.
Mapema mwanzo wa wiki Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa alibainisha kuwa siku ya tarehe 9 Disemba
itakuwa siku ya kutathimini kazi ya usafi inayoendelea kufanyika ndani ya Mkoa,
pia utafanyika usafi kwenye maeneo ya huduma za jamii kama masoko na
Hospitalini.
Maagizo yaliyotolewa wakati wa
kupanga mikakati ya utekelezaji wa agizo la kufanya usafi kwenye Mkoa wa Dodoma
ni pamoja na mamlaka za serikali za mitaa katika ukaguzi na usimamizi wa zoezi
la usafi kwenye maeneo ya makazi na shughuli
mbalimbali wafanye ukaguzi wa vyoo.
Vilevile ukaguzi kwa kazi
iliyofanyika ya usafi wa mazingira ya makazi, maeneo ya huduma za jamii, maeneo
ya utupaji taka. Maelekezo mengine ni pamoja na matumizi ya sheria ndogo kama
kutoa ILANI, Makatazo na adhabu za Faini kwa makosa ya uchafuzi wa mazingira.
Uongozi wa Mkoa wa Dodoma
umeelezea kuwa zoezi hili la kufanya usafi wa mazingira kila siku na usafi wa
pamoja wa kila siku za jumamosi utasaidia kupunguza magonjwa mengi yatokanayo
na uchafu wa mazingira kama vile kipindupindu, kuhara na magonjwa mengine ya
milipuko na kwa sasa wanasubiri Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kutoa
ratiba ya zoezi la usafi la Jumamosi ijayo ya Disemba 5, 2015.
No comments:
Post a Comment