MAONI YA MH.ZITTO ZUBER KABWE. - LEKULE

Breaking

23 Nov 2015

MAONI YA MH.ZITTO ZUBER KABWE.



"Simtambui Dkt. Shein kama Rais wa Zanzibar, nataka tu kuweka rekodi sawa. Nilimpinga Dkt. Ali Mohamed Shein hadharani na bungeni.Alipoingia Shein bungeni sikusimama kama inavyotakiwa. Nilikaa chini kupinga uhalali wake. Alipoingia Rais John Magufuli nilisimama na kumpa heshima yake kama Rais na kukaa kumsikiliza. Kuendelea kuzomea wakati Rais halali kaingia Bungeni kuzindua Bunge ili wabunge waanze kazi ni kutokuwa na mikakati sahihi. Ilitosha kumzomea Shein na kukaa chini bila kusimama alipoingia kama tulivyofanya. Wenzangu hawakujua pa kuishia. Magufuli anapambana na rushwa. Mimi napambana na rushwa. Namuunga mkono katika vita dhidi ya rushwa.
Anayempinga Magufuli kwa vyovyote vile anatetea wala rushwa na mafisadi. Anayempinga Magufuli ni yule anayeogopa viwanda na mashamba yaliyobinafsishwa kurudishwa Kwa umma"..Ameandika hivyo Mh. Zitto Kabwe
Nini maoni yako?

No comments: