15 Nov 2015

Makamu wa Rais awapa moyo wachezaji wa Taifa Stars kuelekea mchezo wa marudiano

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishangilia sambamba na baadhi ya Viongozi bao la kwanza la Taifa Stars lililofungwa na Elias Maguli, katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia dhidi ya Algeria uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.  (Picha na OMR).
1B
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza Nahodha wa Timu ya Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Canavaro’, baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza mchezaji wa Timu ya Taifa Stars, Thomas Ulimwengu, baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.  Kulia ni Mbwana Samatta, akibugujikwa na machozi.
5

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji mchezaji wa Timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta, baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Baada ya mchezo huo Samatta, alionekana kubugujikwa na machozi muda wote. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.

No comments:

Post a Comment