Karibu Music Festival 2015 laanza kwa kishindo, Ras Six, Msafiri Zawose, Hard Mad, Kokodo band wafunika - LEKULE

Breaking

7 Nov 2015

Karibu Music Festival 2015 laanza kwa kishindo, Ras Six, Msafiri Zawose, Hard Mad, Kokodo band wafunika

DSC_0641
Mwanamuziki wa nyimbo za asili za Kabila la Kigogo, Msafiri Zawose akiimba kwa kutumia  zeze maarufu la Kabila hilo katika shoo yao ya ufunguzi   wa Tamasha la Karibu Music Festival msimu wa pili lililoanza jana Novemba 6.2015. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog)
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[BAGAMOYO-TANZANIA] Tamasha kubwa la Kimataifa la Muziki la ‘Karibu Music Festival’ linaloratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd  ambalo ni la msimu wa pili mwaka  huu usiku wa jana Novemba 6, limeanza kwa kishindo huku wasanii mbalimbali kutumbuiza na kukonga nyoyo.
Baadhi  ya wasanii hao ni pamoja na : Kokodo Band, Tongwa Ensembe, Ze Spirit, Msafiri Zawose na bendi yake. Wengine ni David Vee kutoka Pakistan,  Brina (Jamaica), Ras Six (Tanzania), Hard Mad na wengineo.
Aidha leo Novemba 7, msanii nguli  wa dansi kutoka nchini Congo DRC, Papa Wemba anatarajiwa kupamba tamasha hilo ambapo atashambulia jukwaa na kundi lake zima. Mbali na Papa Wemba wasanii wengine watakaoshambulia jukwaa leo ni pamoja na  Sarabi Band,(Kenya), Bo Denim (Afrika Kusini)  Damian Soul, Jhikoman, na kundi la Weusi (Tanzania).
Tamasha limeandaliwa na Kampuni ya watayarishaji wa muziki ya Legendary kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precion Air, Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets.
KMF ni sehemu ya kukutanisha wadau wote wa muziki kutoka dunia nzima, kubadilishana uzoefu wa kikazi na kufungua milango kwa wasanii kukuza mtandao wa marafiki na kujifunza vitu vipya toka wasanii wa  ndani na nje ya nchi.  Wasanii wote wanaotumbuiza tamasha hilo  muziki wao wanapiga ‘live’ kwa vyombo vya bendi na hakuna matumizi ya CD ‘playback’.
DSC_0637
Wasanii wa kundi la Msanii Zawose wakitumbuiza kwenye tamasha hilo la Karibu Music Festival msimu wa pili  jana Novemba 6.
DSC_0656
DSC_0555
DSC_0589
Msanii Ras Six
DSC_0556
kundi la David Vee 
DSC_0623
Msafiri Zawose katika ubora wake..
DSC_0545

Host wa Karibu Music Festival wakishoo love muda mfupi wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo..

No comments: