Mtendaji
Mkuu wa Afrika Mashariki wa kampuni ya Letshego, Bwana Tom Kocsis
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
utambulisho mpya wa kununua hisa asilimia 75 za benki ya Advans
Tanzania. wengine ni maafisa waandamizi wa kampuni hiyo (Picha zote na
Andrew Chale).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
Kampuni
ya LETSHEGO Holding Limited yenye makao yake makuu nchini Botswana
ambayo kwa Tanzania ikijulikana kama taasisi ya Mikopo ya Faidika,
imetangaz kupata asilimia 75 ya hisa kutoka katika benki ya Advans ya
Tanzania kwa kununua hisa moya kwa shilingi Bilioni 15.5 ambazo ni sawa
na dola za Kimarekani Milioni 7.
Wakizungumza
mbele ya waandishi wa habari mapema jana jijini Dar es Salaam, viongozi
wakuu wa Faidika na Advans Tanzania wamebainisha kuwa sasa huduma za
kifedha nchini zimeongezeka maradufu hivyo ni fursa za kipekee kwa
watanzania wakiwemo wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kuchangamkia
huduma katika benki hiyo ya Advans.
"Kufanikiwa
kwa Faidika, kunaongeza uwekaji wa akiba, malipo, mikopo ya biashara
ambayo ni moja ya mikakati yetu kwa wateja wetu. Hii pia itaruhusu benki
ya Advans kutoa mchango mkubwa kwa Serikali ya Tanzania" ameeleza
Mkurugenzi Mkuu wa Letshego Group, Chris Low katika tukio hilo.
Mkurugenzi
huyo ameongeza kuwa, Benki kuu ya Tanzania (BOT) imeipatia kibali
taasisi hiyo ya Faidika kuwa wakala wa benki ya Advans wa kutoa huduma
za kibenki kwa niaba ya benki hiyo, katika vituo takribani 105.
Hata
hivyo Letshego inaamini kuwa mafanikio hayo ni ishara tosha ya kutoa
huduma bora kwa watu wote ikiwemo wale wa kipato cha chini, kati katika
jamii ambao kihistoria hawajaweza kupata huduma stahiki katika benki za
biashara hivyo mfumo mzuri wa kuwezesha jamii kupata huduma za kifedha,
Letshego imekuja wakati muafaka wa kusaidia Serikali kuinua uchumi.
Letshego/Faidika
kwa Tanzania inatoa huduma zaidi ya Watanzania 44,000 kupitia taasisi
yake hiyo ya mikopo ya Faidika huku bidhaa na huduma zake pia
zikipatikana kupitia mitandao wenye matawi zaidi ya 105 na ofisi za
Satelaiti huku ikiwa na timu ya maafisa mauzo wapatao 230.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Advans Tanzania, Bwana Tanguy Gravot (wa kwanza kulia)
akizungumza kwenye mkutano mkutano huo. Wengine ni maafisa kutoka
kampuni ya Letshego ambao wamenunua hisa asilimia 75 kwa benki hiyo ya
Advans Tanzania.
Kwa
upande wao benki ya Advans Tanzania wamepongeza kampuni ya Letshego kuwa
mbia mkuu wa benki hiyo kwa njia ya uuzwaji wa hisa. Kwa hatua hiyo
Letshego atakuwa mwanahisa mkuu huku wale wanahisa waanzilishi wa benki
hiyo wakiwemo Advans SA na FMO watabaki kuwa wanahisa wadogo wa kampuni.
"Umoja
ulioundwa kati ya kampuni hizi mbili utaiwezesha benki ya Advans
Tanzania kutoa huduma zilizo bora kwa wateja wote wakiwemo wale wadogo,
wa kati na wakubwa kwa maeneo yote huku pia kuongeza wigo wa kijiografia
za huduma." alieleza Mkurugenzi Mtendaji wa Advans SA, Bw. Claude
Falgon.
Kwa hatua hiyo, Advans inaamini kuwa wajasiriamali waadogo na wa kati ni wakati wa kuchangamkia fursa zaidi katika benki hiyo.
Advans
ya Afrika Kusini (Advans SA) ni kampuni iliyoundwa tokea mwaka 2005 na
Developement Finance 9Horus) pamoja na Eid,KfW, FMO, CDC Group plc, AFD
group na IFC huku shughuli yake kubwa ikiwa ni kutengeneza mtandao wa
taasisi ndogo ndogo za kifedha (MFIs) katika nchi zinazoendelea na
zinazoinukia ilikutoa huduma za kifedha kwa wajasiliamali wadogo na wa
kati.
Mtandao wa Advans umesambaa karibu dunia nzima ambapo pia waweza kutembelea mtandao wa : www.advansgroup.com
Mkurugenzi
Mkuu wa Letshego Group, Chris Low (katikati) akifafanua jambo kwa
wanahabari (hawapo pichani) wakati wa shughuli hiyo ya kutangaza kuingia
ubia na benki ya Advans Tanzania.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia shughuli hiyo.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia shughuli hiyo.
Mmoja wa wajumbe wa Bodi wa Taasisi ya mikopo nchini ya Faidika, Dk.Ellen Otaru Okoedion akielezea fursa za mikopo inayotolewa na Faidika huku akitumia wasaha huo kuwaomba wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kuchangamkia huduma za kibenki na mikopo zinazotolewa na Faidika pamoja na benki ya Advans Tanzania.
No comments:
Post a Comment