Joto la utawala wa Rais John Magufuli limebadili utendaji kazi wa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali waliozoea kukaa ofisini na sasa wanafanya kazi nje ya ofisi na kusikiliza kero za wananchi kwenye maeneo yao.
Wakati
hilo likifanyika, Ikulu jijini Dar es Salaam imesema katibu mkuu au
mtumishi yeyote wa umma atakayeshindwa kwenda na kasi na mabadiliko ya
utendaji kazi katika serikali ya awamu ya tano ajiondoe.
Tamko
hilo linalotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue,
alipohojiwa jana kuhusu kutokuwapo kwa makatibu wakuu wa wizara kadhaa
kwenye ofisini zao wiki iliyopita.
Makatibu wakuu wa Wizara kadhaa wamelazimika kuzifunga ofisi zao na kuelekea mikoani kusikiliza kero za wananchi.
Makatibu wakuu wa Wizara kadhaa wamelazimika kuzifunga ofisi zao na kuelekea mikoani kusikiliza kero za wananchi.
Hali
ya viongozi hao kuhama jiji na kwenda mikoani imeleta mabadiliko ya
utendaji kazi wao baada ya miaka ya nyuma kuzoeleka kutumia muda mwingi
ofisini na kuacha kazi za nje kufanywa na waziri, naibu au watendaji
wengine.
Baadhi
ya wizara ambazo zilitembelewa na kukuta ofisi za katibu mkuu zikiwa
zimefungwa ni Uchukuzi, Tamisemi, Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano na
Ujenzi.
Baadhi
ya wafanyakazi wa wizara hizo ambao hawakutaka majina yao yatajwe,
walisema mabosi wao kwa sasa inakuwa nadra kuonekana ofisini wakifanya
kazi kwa kuogopa kuonekana wazembe.
"Hatujawahi
kuona katibu anakwenda mikoani kama ilivyo sasa, kila siku anakwenda
huku na kule kuangalia miradi na kero za wananchi," alisema mmoja wa wafanyakazi wa moja ya wizara hizo.
Akitoa
kauli ya serikali, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema
kuanzia sasa katibu Mkuu na mtendaji wa serikali ambaye anafanya kazi
kwa kusuasua ajiondoe mwenyewe.
Alisema
tayari amefanya kikao na makatibu wote kuwaeleza suala hilo na
atakayerudi nyuma hatakuwa na nafasi katika serikali ya awamu ya tano.
"Jambo
hilo tumekubaliana kwenye kikao, serikali ya awamu ya tano haitakuwa na
utani kwa wale watakaoonekana hawaendi na kasi ya Rais, sasa wanatakiwa
kuchagua kama wanataka kuendelea na nafasi zao au la," alisema Sefue
No comments:
Post a Comment