Baadhi
ya wananchi wilayani Chato wameipongeza serikali kupitia mpango wa
TASAF Awamu ya tatu wa kunusuru kaya masikini.
Wakiongea kwa nyakati Tofauti wananchi hao kutoka kata ya Bwongera ambao
ni wanufaika wa Mpango huo wamesema Mpango wa TASAF Awamu ya tatu ni
mkombozi kwa wananchi masikini na wameahidi kutumia pesa hizo kwa
manufaa ya familia na mahitaji muhimu ya huduma za afya na elimu kwa
watoto wao.
“Tunaishukukuru
serikali yetu kwa huu mpango mzuri ambao matunda yake tunayaona hapa
hapa, nimepokea hela mwezi uliopita nimenunua mbuzi watatu, malipo ya
awamu hii nitaboresha nyumba yangu” alisema Bibi Tabu Paulo mkazi wa
kijiji cha Mkolani kata ya Bwongera.
Kwa
upande mwingine baadhi ya wanufaika wa mpango huo wamelaumu baadhi ya
akina baba ambao wamekuwa wakiwalazimisha wenzi wao kutokwenda kuchukua
fedha hizo na badala yake wakina baba ndiyo wamekuwa wakitaka
kukabidhiwa fedha hizo ambapo ni kinyume na mwongonzo wa mpango wa TASAF
awamu ya tatu ambao unawataka wakina mama kama wawakilishi wa kaya
wapokee fedha hizo kwa niaba ya familia.
Mratibu
wa TASAF wilayani Chato Bw. Alex Manga’ra amesema tangu kuanza kwa
zoezi la ulipaji fedha kupitia mpango huo wamekutana na changamoto hiyo
ambapo amesema utaratibu wa nani anapaswa kupokea fedha hizo tayari
ulikwishaelezwa kwenye mikutano ya serikali za vijiji na mikutano mikuu
ya vijiji vyote vinavyonufaika na mpango huo lakini akina baba wamekuwa
wakitaka kulipwa wao badala ya akina mama. Hata hivyo Bw. Manga’ra
ameahidi kuendelea kutoa elimu kwa wanufaika wa mpango ili tatizo hilo
lisiendelee kujirudia.
Naye
Msimamizi Mshauri wa Mpango kutoka TASAF Bw. Richard Komba ameziomba
kaya zinazonufaika na mpango kutokufumbia macho pindi waume zao
wanapowakataza kwenda kupokea fedha hizo na kuwataka wawasiliane na
wawakilishi wa serikali ya kijiji ambao wamo kwenye mpango ili hatua za
haraka ziweze kuchukuliwa.
Mpango
wa TASAF Awamu ya tatu ulizinduliwa mwezi January 2014 na aliyekuwa
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Rodrick Mpongolo na mchakato wa kubaini
kaya masikini ulianza mapema mwaka huu ambapo kaya Zaidi ya 8000 kutoka
vijiji 71 wilayani hapa ziliibuliwa na kuthibitishwa kupitia mikutano
mikuu ya vijiji na Hatimaye kukidhi vigezo vya kaya masikini.
Bibi
Tabu Paulo mkazi wa kijiji cha Mkolani kata ya Bwongera ambaye baada ya
kupokea fedha za awamu ya kwanza kupitia mpango wa TASAF III alinunua
mbuzi 3 kama njia ya kujikwamua na umasikini.
Bibi
Sesilia Bernado (kulia) mkazi wa kijiji cha Mkolani kata ya Bwongera
ambaye baada ya kupokea fedha za awamu ya kwanza kupitia mpango wa TASAF
III alinunua mabati 6 ili aboreshe makazi yake.
Bibi
Maria John (anayehesabu fedha) ambaye ni miongoni mwa wakazi wa kijiji
cha Bwongera aliyechaguliwa na mkutano mkuu wa kijiji kuwa mlipaji wa
fedha kwenye mpango huo kupitia kijiji hicho akihesabu fedha tayari
kumkabidhi Bibi Tabiza Nusu wa kijijini hapo.
Bw.
Richard Komba (aliyesimama juu ya meza) ambae ni msimamizi mshauri wa
mpango wa TASAF III akieleza jambo kwa wanufaika wa mpango wa kjiji cha
Kikumbaitale kata ya Kigongo wilayani hapa.
Baadhi ya wanufaika wa mpango wa kijiji cha Mkolani kata ya Bwongera wakisubiri malipo yao kupitia mpango huo.
wanafunzi
wa MEMKWA katika shule sitili ya Katete ambao hapo awali walishindwa
kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa sare za
shule na madaftari lakini kupitia mpango wa TASAF III wameweza
kuendelea na masomo shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment