JESHI la Polisi mkoani Tanga limemfukuza kazi askari wa kikosi cha usalama barabarani aliyetambulika kwa namba F. 785 CPL Anthony Temu (46) wa kituo cha Polisi Kabuku kwa kosa la kufedhehesha jeshi hilo.
Akitoa taarifa kwa vyombo ya habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Zuberi Mwombeji amesema askari huyo amefukuzwa baada ya kuthibitishwa kwa taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiomba na kupokea rushwa wakati akitekeleza majukumu yake.
No comments:
Post a Comment