Aliyekuwa
Spika wa Bunge la Kumi, Anne Makinda ameamua kukaa kando ya mbio za
Uspika wa Bunge la 11, siku chache baada ya kufanya kampeni kuwania
nafasi hiyo kwa mara nyingine.
Taarifa
za kuaminika zimeeleza kuwa Mama Makinda aliamua kuchukua uamuzi huo wa
kujiweka kando ya mchuano huo baada ya kushauriwa na watu wake wa
karibu kufuatia dalili walizoziona kwenye mchakato huo pamoja na mambo
mengine.
Awali
mama Makinda alidaiwa kuanza kampeni kupitia ujumbe mfupi alioutuma kwa
wabunge wateule kupitia simu za mkononi akiwapongea na kuwaomba
kumuunga mkono kuwa Spika wa Bunge la 11.
“Mimi
ndugu yako kwa unyenyekevu na heshima kubwa kwa ko kama mbunge wangu,
naomba kugombea uspika kwa mara nyingine, kwa msaada w Mwenyezi Mungu
nakutegemea sana naomba uniunge mkono. Asante kwa ukarimu wako,”
ilisomeka sehemu ya ujumbe unaoaminika kuwa ulitumwa na Anna Makinda kwa
wabunge wateule.
Hata
hivyo, hadi pazia la kuchukua na kurudisha fomu za kuwania Uspika wa
Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linafungwa, Mama Anna
Makinda alikuwa hajarudisha fomu yake hivyo kuonesha dhahiri kuwa
ameachana na mpango huo.
Makada
21 wa CCM wamejitokeza kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge.Dkt. Emmanuel
Nchimbi, Samwel Sitta, Dkt Didas Masaburi, Balozi Philip Marmo, Mussa
Hassan ‘Zungu’, Job Ndugai, Abdallah Mwinyi ni miongoni mwa majina ya
makada wa CCM waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment