Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemkuta na hatia aliyekuwa
Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la Taifa (ATCL), Bw. David Mattaka na
wenzake wawili baada ya mashahidi 13 kutoa ushahidi wao mahaakamni hapo.
Hakimu
Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Emmilius Mchauru amesema mahakama
imejiridhisha bila shaka baada ya upande wa mashitaka kuwasilisha
mashahidi 13 kuhusu tuhuma zinazomkabili kigogo huyo wa zamani wa ATCL
za matumizi mabaya ya ofisi kwa kutanagza zabuni ya ununuzi wa magari
yaliyochakaa 26 na kuisababishia hasara serikali ya mabilioni ya
shilingi.
Washitakiwa
wote watatu wakiongozwa na mawakili wao walikubali kutoa ushahidi wao
kwa kula kiapo ambapo mashahidi wa washitakiwa hao wanatarajiwa kuanza
kuwatetea mapema Desemba 10 na 11 huku dhamana zao zikiendelea.
Katika
shauri hilo la matumizi mabaya ya ofisi linawakabili David Mattaka
aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa
ATCL na Elsaph Ikomba na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani, Wiliam Haji
No comments:
Post a Comment