Rais wa Mexico Pena Nieto
Utafiti
ulioendeshwa nchini Marekani unaonyesha raia wengi wa Mexico wanaondoka
kwenye taifa hilo kubwa zaidi ulimwenguni ukilinganisha na idadi ya
wanaoingia nchini humo,tofauti na hali ilivyokuwa nusu karne iliyopita.
Utafiti
huo uliofanywa na kituo cha utafiti cha Pew umeeleza kwamba katika
kipindi cha miaka mitano mfululizo mpaka kufikia mwaka wa jana,
inakadiriwa Wamexico milioni moja wakiwa na familia zao wameondoka
nchini Marekani na kurejea nchini Mexico.
Katika
kipindi kama hicho,wa Mexico elfu moja na arobaini waliondoka nchini
mwao kuelekea Marekani kutafuta makazi bora.kituo hicho cha utafiti
kinatanabahisha sababu kubwa ya kurejea nyumbani kwa wa Mexico, ni ile
hamu ya kutaka kuungana na familia zao.
Ripoti
hii imetolewa wakati huu ambapo wimbi la wahamiaji kuingia nchini humo
likiwa limeongezeka katika kampeni za urais nchini Marekani .
Mgombea
mmoja kutoka upande wa chama cha Republican , Donald Trump, ametoa wazo
la kujengwa kwa ukuta kati ya Mexico na Marekani kwa misingi ya kuzuia
uhalifu unaofanywa na wa Mexico pamoja na usafirishaji dawa za kulevya
kutoka Mexico na kuziingiza Marekani.BBC
No comments:
Post a Comment