Kutoka Hospitali ya Mnazi Mmoja, taarifa ni kwamba wamepokelewa watu watatu waliojeruhiwa, wawili kati yao wakiwa wamepigwa risasi ambapo mmoja tayari anafanyiwa operesheni baada ya risasi kupitia ubavuni kuelekea ubavu mwengine.
Ripoti kutoka eneo la Jang'ombe zinaeleza kuwa vikosi vya usalama vilipita eneo hilo na kuwashambulia vijana waliokuwa wamejikusanya mitaani.
Chanzo : DW Swahili
No comments:
Post a Comment