MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William Lukuvi
Na Fredy Mgunda,Ismani
MGOMBEA ubunge
wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William
Lukuvi amembeza mgombea mwenzake anayegombea ubunge kwenye jimbo hilo
kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema Patrick Olle Sosopi na
kusema kuwa Sosopi hata afanye hawezi kuvaa viatu vyake kwa kuwa mbunge
wa jimbo hilo.
Kauli ya
Lukuvi aliitoa juzi wakati akiwahutubia wananchi wa vijiji vya
Igingilanyi, Kising’a, Kinywang’anga, Mkungugu, Matembo na Ilambilole
vilivyopo tarafa ya Isimani katika Jimo la Ismani alisema kuwa Sosopi
hawezi kuvaa viatu vyake kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa maana hana
staha ya kuweza kuwashawishi wananchi kuwaletea maendeleo na badala yake
anawabeza wagombea wa chama cha mapinduzi CCM pamoja na mgombea ubunge
wa jimbo hilo kwa kusema kuwa kwa kipindi cha miaka 20 ya ubunge wa
Lukuvi hakuna maendeleo yoyote yaliyofanywa na chama hicho.
“Mimi
kiatu change navaa namba nane Sosopi anavaa namba moja hivi kweli
ataweza kuwa mbunge wa jimbo hili?alihoji huku akishangiliwa sana na
wananchi hao,kiukweli niwaambie kama mnataka maendeleo kichagueni CCM
ndicho chama pekee kitakachowaletea maendeleo na sio chama
kingine.”alisema Lukuvi
Akiwa
katika kijiji cha Kinywang’anga Lukuvi aliahidi kuwatafutia wananchi hao
madaktari wa kutosha kwenye zahanati zilizopo kwenye jimbo hilo pamoja
na dawa za kutosha ili kuendeleza huduma nzuri ya afya kwenye jimbo
lake.
Alisma
kuwa akatika kuendeleza kuduma nzuri ya afya tayari ameagiza gari ya
kubebea wagonjwa(Ambulance) nchini Japani yenye gharama ya Tsh.mil 120
kwa ajili ya zahanati ya kijiji cha Kinywang’anga.
Alisema
kuwa kwa sasa tayari ujenziwa zahanati ya kisinga unaendelea na
wanajenga wodi ya watoto,wodi ya wazazi pamoja na nyumba za kuishi
watumishi ikiwa maendeleo yote yameletwa chini ya uongozi wa CCM.
Alisema
kwa kipindi cha miaka miatano ijayo atahakikisha wananchi wake wanapata
maji ya uhakika kutoka Jimbo la Iringa mjini ambayo yanatokana na Mto wa
Ruaha.
“ Tayari
fedha za kuvuta maji yam to Ruaha kutoka Iringa mjini hadi Ismani
tumeshapata,wataalamu tayari wapo na wamesema muda wowote kuanzia sasa
zoezi la maji Ismani litaanza”alisema Lukuvi
Aliongeza
kuwa uongozi wa serikali ya magufuli hata kabla ya kuamua kugombea
Urais tayari alishaweka mpango wa kutengeneza barabara ya
Kising’a,Ilambilole,Mikongwi,Ngano hadi Ismani tarafani kwa kiwango cha
lami yenye urefu wa Km.35 kwa gharama ya zaidi ya Uro milioni tano
ambapo tayari ujenzi huo umeshaanza.
Wakati
akihutubia wananchiwa kijiji cha mkungugu alisema kuwa atahakikisha
atapandisha kiwango cha elimu kwenye jimbo hilo pamoja na kuweka haki
sawa kwa wanawake na wanaume katika kumiliki ardhi.
Hata
hivyo alisema kuwa suala la umeme kwenye jimbo hilo kwa baadhi ya maeneo
ni la muhimu kwa sababu kuna maeneo yaliyopo ndani ndani hayana umeme
hivyo atahakikisha ataleta nguzo kwa haraka ili wananchi hao waweze kuwa
umeme.
“
Nitawapigania kuhakikisha umeme unaingia kwenye vijiji vilivyojificha
sana ndani ndani na nawaambia lazima nitawaletea nguzo kwa maana mimi
mwenyewe jambo la nguzo sitoshindwa.”alisema Lukuvi
Hata
hivyo aliwataka wananchi hao kumchagua mgombea urais wa CCM John
Magufuli,mgombea ubunge Williamu Lukuvi pamoja na mgombea udiwani wa
kata ya kising’a Ritta Malagala ili waweze kuwaletea maendeleo ya jimbo
hilo na sio mtu mwingine.
Alisema
kuwa kwa uongozi wa Magufuli yeye hataki mchezo huu ni wakati wa kazi na
sio lelemama na kama kutakuwa na kiongozi ambaye ataonesha amekaa
legelege lazima atanyooka kwa maana magufuli hapendi mtu ambae sio
mchapa kazi.
No comments:
Post a Comment