Watu sita wamefariki dunia papohapo baada ya gari waliokuwa wakisafiria aina ya Noah kugongana uso kwa uso na basi. - LEKULE

Breaking

31 Oct 2015

Watu sita wamefariki dunia papohapo baada ya gari waliokuwa wakisafiria aina ya Noah kugongana uso kwa uso na basi.

Watu sitawamefariki dunia papo hapo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya toyota Noah iliyo kuwa ikitokea mikumi kwenda Morogoro  kupasuka tairi ya mbele upande wa kulia na kuanza kuyumba barabarani kisha kugongana uso kwa uso na basi mali ya kampuni ya Princes Muro katika eneo la mbuga ya taifa Mikumi.
Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Lenard Paulo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ajali hiyo  imetokea majira ya saa tano asubuhi ndani ya hifadhi ya taifa mikumi kilometa tatu kufika geti la kutokea ndani ya hifadhi hiyo nakusababisha ajali hiyo iliyo sababisha vifo hivyo vya watu sita wakiwemo wanawake wawili na wanaume wanne na miili imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.
 
Aidha kamanda Paulo amewataka madereva wanao endesha vyombo vya moto kuwa makini na kuendesha magari kwa mwendo wa taratibu hasa wanapokuwa katika maeneo ya mbuga za taifa kwani sheria haziruhusu mwendo kasi ambapo amesema dereva wa basi anashikiliwa na jeshi la Polisi.

No comments: