Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu.
Mahmoud Ahmad Arusha
Jumla
ya watu 27 waliripotiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa kipindupindu huku
kati yao 6 walithibitishwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu. Na watano
wamelazwa katika kituo cha Afya Levolosi.
Akizungumza
na wanahabari ofisini kwake Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu
aliwataka wakazi wa jiji la Arusha kufuata kanuni za ugonjwa huo na kuwa
waepuke kula vyakula sehemu zisizofaa.
Nkurlu
alisema kuwa kwa zaidi ya miezi miwili sasa maeneo mbali mbali hapa
nchini yameripitiwa kuwa na ugonjwa huo katika mikoa ya Dar es
salaam.Morogoro,Pwani na mkoa wa Jirani wa Kilimanjaro mnamo mwezi wa
nane mwaka huu.
Alisema
kuwa aidha katika siku za hivi karibuni mikoa ya Singida na Shinyanga
nayo iliripotiwa kuwa na ugonjwa huo na mgonjwa wa kwanza kuripotiwa
mkoani hapa ni kutoka mkoani Sngida na alilazwa na kupatiwa matibabu na
kuruhusiwa kwa kuanza kutapika na kuharisha akiwa njiani kuja Arusha.
Alitanabaisha
kuwa wagonjwa walioripotiwa wanatoka katika Mkoa wa Singida
watatu,mmoja anatoka halmashauri ya Arusha dc,mmoja kutoka halmashauri
ya Simanjiro na wagonjwa 22 wanatokea hapa jijini Arusha,
“Nawasihi
wakazi wa jiji la Arusha kutambua kuwa ugonjwa wa Kipindupindu umeingia
hapa jijini kwetu na hivyo mfuate maagizo ya wataalamu wa Afya kuepuka
kula vyakula visivyochemshwa na vilivyo kwenye mazingira machafu kuepuka
kupata maambukizi ya ugonjwa wa kipindu pindu”alisema Nkurlu’
Pamoja
na ukweli kwamba ugonjwa wa kipindupindu unatibika hasa mgonjwa
anapowahi matibabu pia inashauriwa wananchi ni vizuri kujikinga na
ugonjwa huo kwa njia za upatikanaji wa maji safi na salama na kunywa
maji aliyochemshwa pia kunawa mikono baada ya kutoka msalani,
No comments:
Post a Comment