WATU 17 WAFARIKI NA WANNE WAKOSEKANA KATIKA MAFURIKO YA PWANI YA AZUR - LEKULE

Breaking

5 Oct 2015

WATU 17 WAFARIKI NA WANNE WAKOSEKANA KATIKA MAFURIKO YA PWANI YA AZUR

Mandelieu-la-Napoule, wilaya jirani ya Cannes, imekumbwa hasa na mafuriko.
Mandelieu-la-Napoule, wilaya jirani ya Cannes, imekumbwa hasa na mafuriko.

Watu 17 wamefariki katika kituo cha magari cha chini ya ardhi kufuatia mafuriko yaliyotokea usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita katika pwani ya Azur, nchini Ufaransa.
Baadhi ya nyumba zimepelekwa na mafuriko hayo, huku raia wakipoteza mali na watu.
Watu kadhaa wamegunduliwa wakiwa hai katika eneo lililokumbwa na mafuriko hayo, zaidi ya kilomita thelathini kutoka pwani ya Mandelieu-la-Napoule katika mkoa wa Nice: vituo vya magari vimeteketea, magari yalifunikwa na matope.
Kadri muda ulivyokua ukiyoyoma, idadi ya watu waliouawa katika mafuriko hayo ndivyo ilivyokua ikiongezeka, "mapak sasa idadi ya watu waliouawa haijakamilika ", Rais wa Ufaransa François Hollande ameonya wakati alipowasili katika eneo la tukio mapema Jumapili mchana Oktoba 4, akiandamana na Waziri wa Mambo ya Ndani Bernard Cazeneuve.
Mpaka Jumapili alaasiri idadi ya watu waliofariki imekua imefikia 17, pamoja na ugunduzi wa mwili wa mwanamke mmoja aliyetoweka katika mji wa Cannes. Mwanamke huyo alifariki katika ajali ya gari ndogo iliyotokea katika wilaya iliyo karibu na Moupin, ajali ambayo ilisababishwa na mafuriko. Watu wengine wanne walitoweka (mmoja katika eneo la Antibes, wawili katika mji wa Cannes nammoja katika eneo la Mandelieu-la-Napoule), amesema Sébastien Humbert, naibu mkuu wa mkoa wa Alpes-Maritimes.
Baadhi ya watu 250 walipewa makazi katika makazi ya muda katika majengo ya wizara moja nchini Ufaransa, huku jumla ya nyumba 11,000 zimekosa umeme katika wilaya tano. Jumatatu, shule 15, chuo na shule ya sekondari zitaendelea kufungwa.