Picha
hii kutoka maktaba inamwonyesha mtoto ambaye anatumika kama askari na
hivyo kumnyima haki yake ya msingi ya kuishi utoto wake, pamoja na
kupata huduma zake za msingi kama vile afya, elimu, malenzi na ukuaji
wenye hadhi. Pamoja na Umoja wa Mataifa kuendelea na kampeni yake ya
kupinga watoto kutumika kama askari, bado taarifa za hivi karibu za
Umoja wa Mataifa, zinaeleza kuwa watoto bado wanaendelea kutumika katika
baadhi ya maeneo kama askari, huku wengine wakiingizwa katika
biashara haramu zikiwamo za ngono.
Vickness
Mayao kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,
akichangia majadiliano kuhusu haki za mtoto wakati wa Mkutano wa
Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kamati iliyokuwa
ikijadili kuhusu haki za mtoto ambapo akizungumza kwa Niaba ya
Serikali Bi. Mayao amesema Serikali inaendelea na uboreshwaji wa
Sheria mbalimbali zinazolinda haki ya Mtoto huku ikisisitiza kwamba
wajibu wa kwanza wa kumlinda mtoto dhidi ya madhara yoyote ni ya
Wazazi wenyewe. aliyekaa nyuma ni Afisa mwingine kutoka Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Grace Mbwilo
.Pamoja
na kufanyika kwa mikutano ya Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa, Mikutano ya Kamati nyingine zikiwamo ya Pili inayohusika
na masuala ya Uchumi na Maendeleo pia imekuwa ikiendelea na vikao
vyake. Pichani (katikati)ni Bw. Ahmed Makame Haji Kamishna wa Tume ya
Mipango kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwa katika moja wa
Mikutano ya Kamati ya Uchumi na Maendeleo wapo pia Bi. Halima Wagao
kutoka Wizara ya Fedha ( ZNZ na Bi. Mtumwa Idrissa kutoka Tume ya
Mipango ( ZNZ)
Bw.
Suleiman Said Ali. Afisa Mambo ya Nje , Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa ( ZNZ) akifuatilia Majadiliano ya Kamati ya Nne
ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, iliyokuwa ikijadili kuhusu masuala
ya misaada ya ulipuaji wa mabomu ya Ardhini, Bw. Ali pia
alishiriki katika Majadiliano ya Umalizwaji wa Ukoloni kwa Makoloni 17
ambayo bado hayajapata fursa ya kujitawala na kujiamulia mambo yake
yenyenyewe likiwamo Koloni la Western Sahara, koloni pekee barani
Afrika.
No comments:
Post a Comment