Mkuu wa
Huduma za Kifedha Kwa Njia ya Mtandao wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Ruan
Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Makao Makuu ya Tigo Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu Wateja wa Tigo
Pesa kupata faida ya robo mwaka ya shilingi bilioni 3.8. Kulia ni Meneja
Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
KAMPUNI
ya Tigo Tanzania imefanya malipo mengine ya gawio la faida ya kila robo
mwaka kwa wateja wake kiasi cha shilingi za ki-tanzania bilioni 3.884.
Hili ni gawio la pili la robo mwaka kwa mwaka huu na ni zaidi ya
asilimia 17 ya bilioni 3.3 ambayo ililipwa na kampuni katika robo ya
pili.
“Lengo
letu ni kuhakikisha wadau wote wa Tigo Pesa wakiwemo wateja binafsi,
mawakala wa rejareja na washirika wetu wa biashara kugawana faida hii
kulingana na kiasi kilichohifadhiwa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa,"
alisema hayo mkuu wa huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel
Haya
ni malipo ya sita katika robo mbalimbali za mwaka ambazo Tigo imekuwa
ikitoa kama faida iliyozalishwa kutoka kwenye akaunti ya Tigo Pesa
ijulikanayo kama Trust inayofanywa na benki kubwa nchini Tanzania.
“Tumefurahi
kwa mara nyingine tena, kwa kutangaza gawio hili kwa wateja wetu
waaminifu wa Tigo Pesa. Malipo haya yanadhihirisha dhamira yetu ya kutoa
huduma za kifedha kwa wateja wetu na nchini kwa ujumla,” alisema
Swanepoel.
Mwezi
Julai, 2014 kampuni ya Tigo ilikuwa ni kampuni ya kwanza ya mawasiliano
ya simu duniani kutoa gawio la faida yake katika akaunti ya Trust,
katika mfumo wa ugawaji wa kila robo mwaka kwa watumiaji wake wa Tigo
Pesa.
Akifafanua
kuhusu malipo, Swanepoel alisema kuwa kabla ya rejesho kwa wateja,
hufanyiwa ukokotoaji kulingana na wastani wa salio la kila siku
lililotunzwa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa. Alitoa mfano wa sababu ya
ongezeko la malipo,kuwayanatokana na ongezeko la jumla ya masalio
katika akaunti ya Trust na wateja zaidi na zaidi kujiunga pamoja
naongezeko la utumiaji waTigo Pesa kwa wateja waliopo.
Mpango
wa utoaji wa faida ni kwa mujibu wa agizo la benki kuu lililotolewa
mwezi Februari mwaka 2014. Hadi sasa kampuni imelipa jumla ya shilingi
za kitanzania bilioni 31.1 tangu kuzinduliwa kwa mpango huu mwaka
uliopita, kwa mujibu wa Swanepoel.
No comments:
Post a Comment