Meneja
Mwandamizi wa Benki Upande wa Taasisi NMB, Noelina Kivaria (kushoto)
akimkabidhi Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawii wa Jamii, Dkt.
Donan Mmbando (kulia) tuzo ya mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kwa
niaba ya wanafunzi nane na walimu wanne bora wa masomo ya biolojia na
kemia.
Meneja
Mwandamizi wa Benki Upande wa Taasisi NMB, Noelina Kivaria akizungumza
wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya
biolojia na kemia kitaifa kidato cha nne na sita katika hafla ya utoaji
tuzo.
Afisa
Mauzo wa NMB, Joseph Mang’ongo akimuonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Aya
na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donald Mmbando kadi ya akaunti ya chapchap
wakati wa maonesho yaliyokwepo katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi
na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa.(P.T)
Wanafunzi
na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa katika hafla ya
kuwakabidhi tuzo kwa kuibuka vinara iliyofanyika mwishoni mwa wiki
katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Picha
ya pamoja ya meza kuu, Uongozi wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na
wanafunzi na walimu katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu
bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa kidato cha nne na sita
jijini Dar es Salaam.
Katika
kutambua jitihada za wanafunzi na walimu nchini, Benki ya NMB
imewatunukia tuzo wanafunzi nane waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo
ya biolojia na kemia kitaifa na walimu wanne waliowawezesha wanafunzi
hao kuwa vinara katika masomo hayo tuzo ya jumla ya shilingi milioni 10
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kila
mwanafunzi aliefanya vizuri zaidi kwenye masomo hayo mawili amejishindia
jumla ya shilingi milioni 1 na kila mwalimu shilingi laki 5.
Meneja
Mwandamizi wa Benki ya NMB Upande wa Taasisi - Noelina Kivaria
alimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando ambaye
alikuwa ni mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Bi.Kivaria
aliwapongeza wanafunzi hao kwa jitihada zao shuleni na kuwaasa
wanafunzi wengine wachukulie hiyo kuwa ni sehemu ya changamoto kwao
hivyo wakaze kamba ili nao waweze kuwa vinara katika masomo yao.
Benki ya
NMB imekuwa ikiipa sekta ya elimu nchini kipaumbele cha hali ya juu kwa
kushirikiana na shule mbalimbali ndani na nje ya Dar es Salaam ikitoa
misaada mbalimbali kama madawati.
Wanafunzi waliotunukiwa tuzo hizo ni:
- Samwel Felician-Nyamanoro Secondary School
- Jenipher Naali-St. Francis Secondary School
- Joshua Zumba-Uwata Secondary School
- Monica Mtei-Marian Girls Secondary School
- Felister Silvester-Ifunda Tech. School
- Mariam Mzingi-Feza Girls Secondary School
- Elisha Mmari-St. Mary Goreti Secondary School
- Innocent Yusufu-Feza Boys Secondary School
Walimu waliotunukiwa tuzo ni:
- Halima Tajiri-Feza Girls Secondary School
- Rogasian Fisso-Uwata Secondary School
- Grolius Rwabutomize-St. Mary Goreti Secondary School
- Jane Lalika-Marian Girls Secondary School
No comments:
Post a Comment