Thomas Sankara
Matokeo
ya ukaguzi wa kimatibabu uliofanyiwa mabaki ya mwili wa aliyekuwa rais
wa Burkina Faso marehemu Thomas Sankara miaka 28 baada ya
kuuawa,yanaonyesha kuwa mwili wake ulijaa risasi kulingana na wakili
aliyekuwa akiwakilisha familia yake kulingana na mtandao wa facebook wa
kituo cha habari cha Burkina 24.
Familia
yake ilikuwa ikingojea matokeo ya DNA kuthibitisha kwamba mabaki hayo
yalikuwa ya bwana Sankara,wakili Benewende Sankara aliviambia vyombo vya
habari nchini humo.
Mariam Sankara mkewe marehemu Thomas Sankara
Bwana
Sankara aliuawa katika mazingira ya kutatanisha akiwa na umri wa miaka
37 na kundi la wanajeshi mwezi Octoba mwaka 1987,na alizikwa kwaa haraka
kufuatia mpainduzi yalioongozwa na mrithi wake Blaise Compaore.BBC
No comments:
Post a Comment