Naibu
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia
(kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na
Michezo Sihaba Nkinga(kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma
wakati wa maandalizi ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru
kinachotarajiwa kufanyika Oktoba 14 katika Uwanja wa Jamhuri mjini
Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta
Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi.
Mfugaji
wa Vipepeo kutoka mkoani Tanga Jane William akitoa ufafanuzi leo kwa
wananchi waliofika katika maonyesho ya wiki ya vijana kwenye Uwanja wa
Barafu mjini Dodoma jinsi ya ufugaji wa vipepeo kwa ajili ya biashara.
Moanyesho hayo ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha Mwenge wa Uhuru
ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Jakaya
Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fissoo akitoa maelezo kwa
Maafisa Utamaduni mbalimbali juu ya hatua wanazozichukua katika kukagua
filamu za kuziwekea madaraja na stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania ili
kujenga uchumi wa Nchi. Maelezo hayo ameyatoa leo mjini Dodoma wakati
wa wiki ya vijana ikiwa ni kuelekea kilele cha Mwenge wa Uhuru ambapo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Jakaya Mrisho
Kikwete atakuwa mgeni rasmi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga
(kulia ) akipata ufafanuzi wa hotuba na maandishi mbalimbali yaliyomo
katika kitabu cha Mwalimu Nyerere cha Freedom and Unity leo mjini
Dodoma wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana . Kushoto ni Afisa Mipango
Msaidizi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Edgar Atubonekisye (kulia) .
Maonyesho hayo yanaenda sanjari na Kilele cha Mwenge wa Uhuru ambapo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Jakaya Mrisho
Kikwete atakuwa mgani rasmi tarehe 14.10.2015 mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment