Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh.
Bernard Membe akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam kushiriki katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa
Mataifa.
Na Mwandishi wetu
JUMUIYA
ya Kimataifa imetakiwa kuwajibika kuhakikisha kwamba wanaweza kuwepo na
amani na usalama kwa kuwa hilo ndilo tatizo kubwa duniani.
Hayo
alisema Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh.
Bernard membe katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa
Mataifa.
Hafla
hiyo imefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja mapema zaidi kuliko tarehe
iliyopaswa ya Oktoba 24 kutokana na Tanzania kuwa katika mchakato wa
uchaguzi.
Waziri
Membe alisema kwamba dunia kwa sasa ipo katika changamoto kubwa ya
usalama kutokana na mizozo inayoendelea katika nchi kadhaa duniani.
Alisema
kumekuwepo na wimbi kubwa la mapigano ndani ya nchi mbalimbali katika
nchi mashariki ya kati, Ulaya na hata Afrika, kukua kwa ugaidi na siasa
za kibaguzi.
“
Sote tunafahamu shida iliyopo katika nchi kama Syria, Iraq, Somalia,
Libya, Afghanistan, Yemen na jamhuri ya Afrika Kati” alisema waziri
Membe na kuongeza kuwa matukio ya vita ya mara kwa mara, misimamo mikali
na ugaidi vimekuwa vikisababisha vifo vingi na mateso kwa jamii.
Kutokana
na hali ilivyo kwa sasa dunia haiko katika hali ya amani na hivyo
juhudi zaidi zinatakiwa kufanyika ili kurejesha amani ambayo ni kiungo
muhimu katika maendeleo.
Pamoja
na kuzungumzia haja ya amani kutokana na dunia sasa hivi kufikia
kiwango cha juu cha wakimbizi ndani na nje ya nchi zao, Waziri Membe
alihimiza mabadiliko katika uendeshaji wa Umoja huo ili kuleta uwiano wa
uwajibikaji kimataifa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh.
Bernard Membe akisalimiana na baadhi ya wakuu wa Mashirika mbalimbali ya
Umoja wa Mataifa nchini huku akiwa ameambatana na pamoja na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula (kushoto).
Mwaka
2005 idadi ya wakimbizi duniani ilikuwa milioni 38 lakini miaka kumi
baadae takwimu zinaonesha kwamba kuna wakimbizi milioni 60 ikimaananisha
kwamba katika kila watu 122 duniani, mmoja ni mkimbizi.Tanzania ina
wakimbizi 169, 874.
Aidha
alisema kwamba bara la Afrika linastahili kuwa na kiti cha kudumu
katika Baraza la Usalama ili maamuzi kuhusu Afrika yawe na mamlaka ya
Afrika yenyewe.
Katika
hotuba yake pia alizungumzia mafanikio ya Umoja wa Mataifa ikiwamo
utengenezaji wa malengo mapya 17 ya maendeleo endelevu na pia ufanisi
katika utekelezaji wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yakifanyakazi kama
kitu kimoja.
Alisifu
mafanikio makubwa yaliyotokana na uongozi wa Mratibu wa Umoja wa
Mataifa nchini Alvaro Rodriguez tangu alipofika nchini miezi 13
iliyopita.
Alisema
utendaji wake unaozingatia ngazi za chini hadi juu na vijijini hadi
mjini umeleta mafanikio makubwa kutokana na kuwa sehemu kamili ya
utekelezaji wa mambo mbalimbali ya maendeleo na kupiga vita umaskini.
Pia
alishukuru mchango wa Umoja wa Mataifa katika kufanikisha elimu ya
uchaguzi hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi ambao utafanyika siku 12
zijazo.
Umoja
wa Mataifa na wadau wake wametoa jumla ya dola za Marekani milioni 22.5
kwa ajili ya shughuli za uchaguzi mkuu nchini na kuimarisha demokrasia
na utawala bora.
Naye
Rais mstaafu Benjamin Mkapa akizungumza katika hafla hiyo alitaka dunia
kutambua kwamba madhumuni ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa bado yapo
palepale na kutaka nchi wanachama kutoa michango yao kuendelea
kupambana na changamoto mpya za dunia katika masuala anuia ikiwamo vita,
umaskini, chakula na mabadiliko ya tabia nchini.
Mkuu
wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji
(UNCDF), Peter Malika akisalimiana na Waziri Membe mara tu baada ya
kuwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
Mataifa
51 yalikutana mjini San Francisco, Marekani baada ya vita kuu ya pili
ya dunia na kuanzisha Umoja wa Mataifa. Wakati wa uanzishaji wa Umoja
huo mataifa manne tu ya Afrika yalikuwepo nayo ni Liberia, Ethiopia,
Misri na Afrika Kusini.
Hata
hivyo rais huyo mstaafu alisema ili Umoja wa Mataifa ufanikiwe ipo haja
ya kubadili mifumo yake ili iweze kuwajibika kikamilifu kwa dunia na
wala si kwa matakwa ya waasisi na matajiri.
Pamoja
na mabadiliko hayo nchi nyingi zinazoendelea zinataka kuwa na haki ya
upigaji kura katika vyombo kadha vya Umoja wa Mataifa ikiwamo shirika la
Fedha na Benki ya Dunia.
Naye
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika hafla hiyo
katika viwanja vya Mnazi Mmoja alisema kwamba Umoja huo utaendelea
kushirikiana na Tanzania katika kuwezesha amani na maendeleo.
Pamoja
na kushukuru kwa wananchi wa Tanzania kuwa pamoja na Umoja wa Mataifa
katika sherehe hizo muhimu sana Dunia nzima, alisisitiza, ushirikiano
kuendelea kuwapo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wadau wa maendeleo, na mashirika ya Umoja wa Mataifa.
“Kwa
kuadhimisha siku hii ya Umoja wa Mataifa kwa pamoja, tunaimarisha
ushirikiano wetu, katika masuala ya msingi, ambayo nchi wanachama wa
Umoja wa Mataifa, wamekubaliana nayo. “ alisema.
Aidha
alizungumzia mapatano ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na Tanzania na
utekelezaji wa mipango ya maendeleo inayoichangiwa na UN nchini Tanzania
chini ya UNDAP na kusema imeleta mafanikio makubwa.
Katika
wiki ya Umoja wa Mataifa, wafanyakazi na viongozi wa serikali, wadau wa
maendeleo na wananchi waliwafanya shughuli mbalimbali zikiwamo za
upandaji miti, usafi na miradi ya nishati mbadala.
Gwaride maalum katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa likitoa heshima kwa mgeni rasmi Waziri Membe (hayupo pichani).
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh.
Bernard Membe akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwenye kilele cha
maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
Waziri
Membe akitoa heshima kwa bendera ya Umoja wa Mataifa ikipandishwa kama
ishara ya kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum akisoma dua kubariki
sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Kiongozi wa madhehebu ya Kikristo akiongoza sala katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Meza
kuu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Celestine Mushy, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William
Mkapa pamoja na mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe wakishiriki sala maalum ya
kuombea amani ya nchi na Umoja wa Mataifa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh.
Bernard Membe akitoa hotuba katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya
Umoja wa Mataifa.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza machache
kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa kabla ya
kumkabidhi tuzo maalum Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mh. Bernard Membe (wa pili kushoto) iliyoshuhudiwa na Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula na Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto).
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimkabidhi Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe tuzo ya Umoja wa
Mataifa iliyotolewa kwa kuzingatia mchango wake katika Maendeleo ya
Milenia (MDGs) na Maendeleo Endelevu (SDGs) katika maadhimisho ya miaka
70 ya Umoja huo jana katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula (katikati) akimpongeza Waziri wa Mambo ya nchi za Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe mara ya kukabidhiwa na
Umoja wa Mataifa kwa kutambua mchango wake katika Maendeleo ya Milenia
(MDGs) na Maendeleo Endelevu (SDGs) katika maadhimisho ya miaka 70 ya
Umoja huo jana katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar.
Meza kuu.
Mabalozi, Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wadau wa Maendeleo pamoja Viongozi wa Serikali wakiwa jukwaa kuu.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja Mataifa
walioshiriki katika kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa
Mataifa.
Maafisa
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulida Hassan
na Eliet Magogo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika viwanja vya
Mnazi Mmoja.
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe hizo.
Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu ya dini.
Meza kuu katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini pamoja na wadau wa maendeleo.
Meza
kuu katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali
walioshiriki kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa
Mataifa.
Meza kuu katika picha ya pamoja na wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
No comments:
Post a Comment