Muonekano
wa nje wa Jengo la Maabara ya Masomo ya Sayansi katika Shule ya
Sekondari ya Bwawani baada ya Mgeni rasmi kuweka jiwe la msingi.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa
maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye Mahafali ya
Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Bwawani.
Baadhi
ya Walimu na Wafanyakazi wa Shule ya Sekondari Bwawani wakifuatilia kwa
makini maelezo ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza kwenye
Mahafali hayo ya Kidato cha Nne.
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Bwawani wakigani shairi lao mbele ya Mgeni rasmi.
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak
Abdulwakil akimkabidhi cheti Mwanafunzi Mhitimu kwenye Mahafali ya Kumi
na mbili ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Bwawani Oktoba 16,
2015(kulia kwa Mgeni rasmi) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John
Casmir Minja.
Baadhi
ya Wahitimu Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Bwawani inayomilikiwa na
Jeshi la Magereza wakipiga makofi wakati wa hotuba ya Mgeni rasmi Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(hayupo
pichani).
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(katikati)
akiwa na Viongozi mbalimbali Meza Kuu wakiimba wimbo wa Shule ya
Sekondari Bwawani kwenye hafla ya Mahafali ya Kidato cha Nne ya shule
hiyo(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir
Minja(wa pili kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Kamishna wa
Magereza wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak
Abdulwakil(kulia) akisoma jiwe la msingi la Jengo la Maabara ya masomo
ya Sayansi kama anavyoonekana katika picha.
WAHITIMU
wa kidato cha nne nchini wameaswa kuachana na fikria potofu kuwa elimu
wanayoipata itawapatia ajira Serikalini au kwenye Sekta binafsi badala
yake watumie elimu hiyo kama nyenzo muhimu ya kuwawezesha kujiajiri wao
wenyewe.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Bw.
Mbarak Abdulwakil alipokuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kumi na
mbili ya kidato cha nne katika shule ya Bwawani Sekondari iliyopo Mkoani
Pwani.
"Katika
hali ya sasa ya utandawazi yapo mambo kadhaa ambayo mtu binafsi anaweza
kuyafanya na kujipatia kipato cha kujiendeleza maisha yake". Alisema
Bw. Abdulwakil.
Bw.
Abdulwakil amesisitiza kuwa wanachotakiwa kufanya wahitimu hao ni
kuyasoma mazingira ya maisha popote watakapokuwa na kuamua namna ya
kujiajiri ili mradi isiwe shughuli zinazopingana na sheria na maadili ya
kijamii, kama vile kuuza madawa ya kulevya, ukahaba, unyang'anyi na
mambo mengine yanayofanana na hayo.
Awali
akimkaribisha Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John
Casmir Minja alisema kuwa uongozi wa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana
na Bodi ya shule utaendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali
zinazozikabili shule hiyo kadri uwezo wa kifedha unavyopatikana.
Jeneral
Minja alizitaja baadhi ya changamoto mbalimbali ambazo tayari
zimefanyiwa kazi ikiwemo miradi ya miundo mbinu ya msingi kama vile
Madarasa, Maabara, Maktaba na mradi wa maji ambapo kwa kiasi kikubwa
miradi hiyo imechangia kuboresha maendeleo ya kitaaluma shuleni hapo.
Kwa
upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Bwawani, Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Emmanuel Lwinga alipokuwa akitoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi
katika mahafali hayo amesema kuwa shule yake ni miongoni mwa shule
nchini ambazo zinafanya vizuri kitaaluma na masuala mengineyo
yasiyoyakitaaluma.
Aliongeza
kuwa mwaka 2014 kati ya wanafunzi 95 waliofanya mitihani ya kidato cha
nne katika shule hiyo wanafunzi 87 sawa na asilimia 91.6% walifaulu,
aidha wanafunzi 52 walichaguliwa kujiunga na masomo ya Kidato cha Tano
katika shule mbalimbali za serikali.
Shule
ya Sekondari Bwawani inamilikiwa na Jeshi la Magereza, ilianzishwa Mwaka
1978 kwa lengo la kutoa elimu ya Sekondari kwa Watumishi wa Magereza
ambapo hivi sasa shule hiyo inatoa elimu kwa vijana wa kike na kiume
kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kuanzia kidato cha kwanza hadi cha
sita.
No comments:
Post a Comment