Mkurugenzi
wa Mipango na Maendeleo ya Biashara, Mhandisi Kato Kabaka (aliyesimama)
kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania, akitoa elimu ya
nishati ya Jotoardhi kwa wafanyakazi wa hifadhi ya wanyamapori Selous na
jinsi gani nishati hiyo itaongeza idadi ya watalii.
Wafanyakazi
wa hifadhi ya wanyamapori Selous na kampuni ya uendelezaji wa Jotoardhi
Tanzania wakimsikiliza kwa makini Mhandisi Kato Kabaka (hayuko pichani)
alipokuwa akiwaelimisha namna nishati ya Jotoardhi itakavyoongeza idadi
ya watalii kupitia mabwawa ya kuogelea ya maji moto yatakayojengwa
ndani ya hifadhi hiyo.
Bwana Eneck Majahasi (aliyesimama) akihitaji
ufafanuzi ikiwa mitambo ya uzalishaji wa nishati ya Jotoardhi itakayojengwa
ndani ya hifadhi ya Selous haitakuwa na madhara kwa wanyamapori walioko ndani
ya hifadhi.
Na. Lilian Lundo - Maelezo
Kuendelezwa
kwa nishati ya Jotoardhi Tanzania itaipelekea kupanda hadhi kwa hifadhi ya
wanyamapori Selous.
Hayo
yalisemwa na Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo ya Biashara, Mhandisi Kato
Kabaka kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania wakati akizungumza na
wafanyakazi wa hifadhi ya wanyamapori Selous, kambi ya Matambwe alipokuwa
akitoa elimu ya nishati ya Jotoardhi yenye viashiria (majimoto) ndani ya hifadhi
hiyo, leo.
“Kama
utafiti utaonyesha chanzo cha nishati ya Jotoardhi kipo ndani ya hifadhi, basi
nishati hiyo itapelekea hifadhi ya Selous kuongeza idadi ya watalii kwa kujenga
mabwawa ya kuogelea yatakayokuwa na maji ya moto na kujenga vibwawa vidogo ndani
ya vibanda vya kupumzikia kwa ajili ya kuweka miguu wageni watakao kuwa
wakitembelea hifadhi hiyo.” Alisema Mkurugenzi Kato.
Mkurugenzi
Kato aliongeza kwa kusema kuwa, mabwawa ya maji moto yatakuwa ni utalii
mwingine ambao utakuwa umeongezeka ndani ya hifadhi ya Selous, kwani watalii
watakapokuja kuangalia wanyama watapata fulsa ya kupumzika ndani ya mabwawa ya
maji ya moto.
Bwana Eneck
Majahasi, mfanyakazi wa hifadhi ya Selous alihitaji ufanunuzi kama hakutakuwa
na madhara kwa wanyamapori ikiwa mitambo ya uzalishaji wa nishati ya Jotoardhi
itajengwa ndani ndani ya hifadhi.
“Kwa sasa
kampuni inafanya utafiiti, utakapokamilika wataalam kutoka Kampuni ya
Uendelezaji Jotoardhi Tanzania na hifadhi ya wanyamapori Selous wataenda
kujifunza namna ambavyo nchi nyingine zimefanikiwa kuzalisha nishati ya
Jotoardhi ndani ya hifadhi za wanyamapori,” Alijibu Mkurugenzi Kato.
Akiongeza
kujibu swali hilo, Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Bi. Johary Kachwamba
alisema kuwa nchi ya Kenya imefanikiwa kuvuna zaidi ya megawati 550 za umeme unaotokana na Jotoardhi na asilimia
kubwa ya mitambo ya uzalishaji ipo ndani ya hifadhi za wanyamapori zilizopo maeneo
ya Olkaria nchini Kenya. Hivyo Tanzania haina budi kujifunza kutoka Kenya na
kufanya vizuri zaidi.
Bwana Tipa
Lazaro mfanyakazi wa hifadhi ya wanyamapori Selous aliipongeza timu nzima ya
Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania kwa elimu nzuri waliyoitoa juu ya
nishati ya Jotoardhi na kusema kuwa wafanyakazi wa hifadhi ya Selous hawana
pingamizi lolote juu ya uendelezaji wa utafiti huo ndani ya hifadhi. Kwani
kukamilika kwa mradi huo ni mafanikio makubwa kwa taifa la Tanzania.
Serikali ya
Tanzania kupitia TANESCO ilisajili kampuni ya kuendeleza nishati itokanayo na
Jotoardhi nchini. Mpaka sasa kampuni hiyo imegundua zaidi maeneo 50 yenye
viashiria vya Jotoardhi hapa nchini. Maeneo hayo yamegawanyika katika kanda
nne, ambazo ni kanda ya kaskazini, kanda ya kusini, kanda ya magharibi na kanda
ya mashariki inayohusisha Utete(Pwani), Luhoi(Pwani) na Kisaki(Morogoro) ilipo
hifadhi ya Selous.
No comments:
Post a Comment