Moto ambao chanzo chake hakijajulikana hadi sasa umeteketeza baadhi ya mabanda ya mama lishe na mitumba karibu na kituo cha mabasi mkoani Njombe.
Hata
hivyo, kikosi cha Zimamoto mkoani humo kimefanikiwa kuuzima moto huo
usiku wa kuamkia leo ambapo polisi wamesema uchunguzi wa tukio hilo
unaendelea.
Kwa mujibu kikosi hicho, mabanda mengine yamesalimika katika ajali hiyo.
Hata
hivyo, kikosi hicho kimewataka wananchi kuwa watulivu wakati huu
wakisubiri matokeo ya uchaguzi ambayo yanatarajiwa kutolewa muda wowote
mkoani humo.
Kwa
mujibu wa kituo cha luninga cha AzamTV, polisi mkoani humo wamesema
uchaguzi mkoani humo ulifanyika kwa utulivu na hsata moto huo
ulipotokea, wananchi wengi walikuwa majumbani mwao.
No comments:
Post a Comment