Baadhi
ya washiriki wa warsha iliyoandaliwa na UNESCO pamoja na Idara ya Mambo
ya Kale wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii Mr Adelhelm Meru kufungua warsha hiyo
iliyofanyika Coral Beach jijini Dar Es Salaam
Baadhi ya viongozi wa Hifadhi wakifuatilia warsha hiyo iliyoandaliwa na UNESCO pamoja na Idara ya Mambo ya Kale
Mwakilishi
wa UNESCO Nchini Ms Zulmira Rodriguez (katikati) akichangia moja ya
mada iliyowasilishwa na baadhi ya wakuu wa hifadhi waliohudhuria warsha
hiyo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dr Adelhelm Meru akifungua
warsha ya siku moja iliyoandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Idara ya
Mambo ya Kale kwaajili ya
kujadili uboreshwaji wa utawala na matumizi endelevu ya hifadhi za
urithi na mazingira za Tanzania, ambazo ni Magofu ya Kilwa; Michoro ya
Asili Kondoa; Mji Mkongwe Zanzibar; Hifadhi ya Wanyama Selous; Hifadhi
za Taifa za Serengeti, Ngorongoro, Lake Manyara na Mlima Kilimanjaro; na
Hifadhi ya Mazingira ya Usambara Mashariki’.
Mkuu
wa Hifadhi ya Kondoa Rock Art, Zuberi Mabie akichangia mada katika
warsha hiyo iliyofanyika jana katika kujadili mafanikio na changamoto
zinazoikabili hifadhi hizo.
Warsha
ikiendelea juu ya utunzaji na uendelezaji wa maliasili na vivutio vya
Utalii iliyofanyika katika hoteli ya Coral Beach jijini Dar Es Salaam.
Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
UNESCO
kwa kushirikiana na Idara ya mambo ya kale imeendesha warsha ya siku
moja kwa wakuu wa hifadhi na vivutio vya utalii hapa nchini huku wakuu
hao wakishirikishana mafanikio na changamoto zinazowakabili katika
hifadhi zao.
Warsha
hiyo iliyohudhuriwa na Wakuu wa hifadhi mbalimbali hapa nchini iliweza
kuhusisha uwasilishaji wa mafanikio na changamoto wanazokutana nazo
wakuu wa hifadhi hizo katika hifadhi huku matatizo makubwa yakiwa ni
Ukosefu wa Pesa kwaajili ya Kujiendesha na Kwa baadhi ya hifadhi kukosa
nyumba za Wafanyakazi na upungufu wa wafanyakazi kwa baadhi ya hifadhi
hizo.
Mbali
na Changamoto hizo pia wakuu wa hifadhi walielezea mafanikio yao katika
hifadhi hizo katika vipengele tofauti tofauti kama Vitendea kazi,
Ujumuikaji wa jamii katika hifadhi hizo, Utalii, Rasilimali watu,
Uhifadhi Utawala na mengineyo.
Moja
ya mafanikio katika nyanja tofauti Mkuu wa Hifadhi ya Usambara Mashiriki
(East Usambara Reserve Management) Bi Mwanaidi Kijazi alisema kuwa
hifadhi yake imetokea kuwa kituo cha Mafunzo kwa wengine na kupelekea
kuanzishwa kwa Amani Nature Reserve na hifadhi hiyo kufanikiwa katika
kutoa taarifa kwa wakati kwa njia ya Vipeperushi kuhusiana na Mradi huo
wa Amani Nature ambao upo kusini mwa Hifadhi hiyo ya Usambara Mashariki.
Vilevile
alisema katika hifadhi yake kuna wafanyakazi ambao wanaweza kuhudhuria
shughuli za Hifadhi hiyo na kusema na hiyo ni moja ya Mafanikio katika
Hifadhi hiyo ya Usambara Mashariki.
Kwa Upande wao UNESCO walisema wataendelea kushirikiana na idara ya Mambo ya Kale katika kutoa ushirikiano na misaada ya kitaalam katika kuhakikisha Hifadhi hizi zinaweza kujiendeleza na kujiboresha na kuvutia watalii zaidi.
No comments:
Post a Comment