Baadhi
ya Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa kutumia Vipodozi wakiwa
kwenye mafunzo kwa njia ya Vitendo..Wanawake wachache wa jiji la Dar es
salaam wameendelea kunufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi
vya LuvTouch Manjano. Washiriki hawa wameendelea kufundishwa matumizi
sahihi na ueledi wa kutumia vipodozi (makeup) mbalimbali kutokana na
nyakati tofauti. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na mtaalamu wa mambo ya
urembo na muasisi wa Taasisi ya Manjano Foundation mama Shekha Nasser.
Mafunzo haya yenye lengo la kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana
na tatizo la ukossefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya
Tasnia ya Urembo
Mafunzo
haya yamegawanywa katika awamu mbili ili kumsaidia mjasiriamali wa kike
kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya Biashara namna ya
kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika Mpangilio wa
Biashara ikiwemo Matumizi sahihi ya Rasilimali Muda, Fedha, Muda na pia
namna ya kujitunzia akiba itokanayo na Biashara yake
Awamu
ya Pili mshiriki anafundishwa Matumizi sahihi ya Vipodozi kuendana na
wakati, mfano office makeup, day, evening na namna ya kumpamba bi
Harusi. Pia wanafundishwa namna bora ya kutumia Vipodozi vya LuvTouch
Manjano kwa lengo ya kuwa kila mshiriki atakayehitimu mafunzo haya aweze
kujiajiri na kujitegemea kwa kuendesha maisha yake ya kila siku kwa
kuwapambamba watu wenye Shuguli Mbalimbali kama vile fashion, sendoff,
harusi nakadhalika
Pamoja
na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwa (paired) na Mwanamke mmoja
mwenye mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii watakaowaita
'Mentor'. Mentor night kama dada wa kumuongoza katika safari yake ya
biashara kwa muda wa mwaka mzima.
Baada
ya Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation
inatoa Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya
Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu
wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea.
No comments:
Post a Comment