Netanyahu alidai Hitler mwanzoni hakutaka kuwaangamiza Wayahudi
Ujerumani imesisitiza kwamba ndiyo inayowajibika kwa mauaji ya Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Hii ni
baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuibua mzozo mkubwa
baada yake kudai kiongozi mmoja wa Wapalestina ndiye aliyewaambia
viongozi wa chama cha Nazi kuwaua Wayahudi barani Ulaya.
Chansela
wa Ujerumani Angela Merkel alisema Wajerumani wanafahamu wazi kwamba
viongozi wa Nazi ndio waliopanga na kutekeleza mauaji hayo yajulikanayo
kama Holocaust.
Netanyahu
alikuwa amedai kiongozi wa Nazi Adolf Hitler alitaka tu kuwafurusha
Wayahudi kutoka Ulaya, lakini Mufti Mkuu wa Jerusalem Haj Amin
al-Husseini akamwambia: "Wachome moto."
Matamashi hayo yamekashifiwa vikali na wanahistoria wa Israel pamoja na wanasiasa.
Akiongea
kando ya Merkel mjini Berlin, Bw Netanyahu alikuwa awali amesema "hakuna
anayefaa kukana kwamba Hitler aliwajibika kwa kutekeleza mauaji ya
Wayahudi".
Lakini
Jumanne katika hotuba ya Baraza Kuu la Wazayuni Duniani mjini Jerusalem,
Bw Netanyahu alidai Husseini ndiye aliyetoa wazo la kuwaangamiza
Wayahudi.
"Hitler hakutaka kuwaangamiza Wayahudi wakati huo – alitaka tu kuwafurusha,” aliambia kongamano hilo.
Matamshi hayo ya Netanyahu yamekashutumiwa vikali na viongozi wa Wapalestina
"Na Haj Amin al-Husseini alimwendea Hitler na kusema: 'Ukuwafurusha, wote watakuja hapa.’
“’Basi nifanye nini nao?’ [Hitler] alimwuliza. Yeye [Husseini] akamjibu: ‘Wachome moto.'"BBC
No comments:
Post a Comment