Hillary Clinton
Anayedhaniwa
kuwa mstari wa mbele katika uteuzi wa Urais katika chama cha
Democratic, Hillary Clinton, amewalaumu wapinzani wake wa chama cha
Republican kwa kutumia vifo vya wanadiplomasia nchini Libya kujinufaisha
kisiasa.
Bi
Clinton amekuwa akitoa ushahidi mbele ya Kamati ya Bunge la Congress
inayochunguza shambulizi katika ubalozi wa Marekani nchini Libya, katika
mji wa Benghazi mwaka 2012 alipokuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni.
Alisema alijiwajibisha kwa kukubali kosa hilo ambapo watu wanne walifariki, kukiwemo balozi Christopher Stevens.
Mwanachama
mkongwe wa kamati huyo kutoka chama cha Democratic, Elijah Cummings,
alisema kuwa uchunguzi huo unaoongozwa na chama cha Republican ni
matumizi mabaya ya sheria yenye lengo la kumvurugia Bi Clinton kampeni
yake ya kutaka kuwa Rais wa Marekani.BBC
No comments:
Post a Comment