Rais wa Ufaransa François Hollande katika Ikulu ya Elysée.
Katika
hali hii ya mvutano kabla ya kura ya maoni nchini Congo-Brazzaville,
Ofisi ya rais wa Ufaransa imetoa msimamo wake mpya juu ya hali inayojiri
nchini humo.
Katika
ndogo ya Ikulu ya Elysée iliyotumwa kwenye vyombo vya habari, François
Hollande amesema " anaunga mkono uhuru wa kujieleza " nchini
Congo-Brazzaville na amekumbusha kwamba alikuwa ametaka, wakati wa
hotuba yake mjini Dakar mwezi Novemba mwaka 2014, kwamba " Katiba
zinapaswa kuheshimiwa ".
François
Hollande amejaribu kujiweka mbali na Denis Sassou-Nguesso. Wakati wa
mkutano wa nchi zinazozungumza Kifaransa mjini Dakar, Novemba 27, 2014,
Rais Hollande alionya kwenyeRFI kuhusu marais ambao wanataka kubadili
sheria kwa kutafuta awamu ya tatu. Hasa, akimaanisha sheria ya kuweka
kikomo kwenye umri, akimlenga Rais wa Congo-Brazzaville Denis
Sassou-Nguesso.
Julai 7,
François Hollande alimpoeka katika Ikulu ya Elysée Rais Denis
Sassou-Nguesso kufuatia baada ya rais huyo kumba kukutana kwa mazungumzo
na Rais wa Ufaransa. Na katikafursa hilo, wawili hao walikubaliana,
katika taarifa yao, kuhusu uwezekano wa kuitisha kura ya maoni ya katiba
kwa misingi ya "makubaliano". Jambo ambalo halikutekelezwa nchini
Congo-Brazzaville.
Kabla ya
Jumatano iliyopita, baada ya kusema kwamba Denis Sassou-Nguesso anaweza
kushauriana na watu wake kuhusu kuitishwa kwa kura ya maoni ya Katiba,
François Hollande aliwashangaza watu wengi hasa waangalizi ambao wameua
wakikosoa msimamo wa Denis Sassou-Nguesso. Jambo ambalo lillisababisha
hisisa mbalimbali kuanzi kwa upinzani wa Congo-Brazzaville hadi nchini
Ufaransa.
Msimamo wakosolewa
Ijumaa
asubuhi wiki hii, chama cha National Front, kupitia sauti ya Louis
Aliot, kimeomba serikali ya Ufaransa kujieleza kuhusu msaada wake kwa
viongozi wa ya Congo-Brazzaville. Louis Aliot pia ameshutumu hatari ya
mabadiliko ya katiba bila ya kuwepo maelewano nchini Congo-Brazzaville.
Somo la demokrasia lililotolewa na chama cha National Front kwa Francois
Hollande kutoka chama cha Kisoshalisti, si la kawaida.
Leo
Ijumaa saa sita mchana, Ofisi ya rais hatimaye imetoa taarifa kwa vyombo
vya habari ambapo Rais wa Ufaransa " amelaani vurugu za aina yoyote,
ameunga mkono uhuru wa kujieleza na amekumbusha kwamba aliwataka wakati
wa hotuba yake mjini Dakar Novemba 29, 2014, viongozi hususan marais
kuheshimu Katiba za nchi zao ". Siku mbili baada ya mkutano wake na
vyombo vya habari katiak Ikulu ya Elysée, François Hollande anajaribu
kujiweka mbali na rais wa Congo-Brazzaville. Kwa sasa Rais Hollande
anajaribu kuweka wazi msimamo wa Ufaransa kwa marais kama Denis
Sassou-Nguesso
No comments:
Post a Comment