Makamu
Mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Hamid M. Hamid (wapili
kushoto) akisoma matokeo ya wagombea nafasi ya Urais jana jijini Dar es
Salaam katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,anayemfuata kulia ni
Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
Baadhi
ya waandishi wa Habari wa Ndani na Nje ya nchi wakifuatilia zoezi la
kutangazwa kwa matokeo ya wagombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
huu jana katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Msaidizi
wa Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema Bw. Matson Chizi akihojiwa na
mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kiswahili, Sauti ya Ujerumani (DW)
Bi.Hawa Bihoga kuhusu namna gani analiona zoezi la utangazaji wa matokeo
linafanyika.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wanne kushoto
kwa waliyokaa katika picha ya pamoja kwa baadhi na waangalizi wa
uchaguzi kutoka nchi za Jumuiya ya SADC walipotembea ukumbi unaotumika
kutangazia matokeo ya wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
jana jijini Dar es Salaam.
Mwandishi
wa habari kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Edward Kondela
akimhoji mmoja wa waangalizi wa uchaguzi ambaye ni Mwenyekiti wa SADC
nchini Malawi Bw.Justice Mbendera alipotembelea ukumbi wa kutangazia
matokeo ya urais jana jijini Dar es Salaam.
Na Beatrice Lyimo-Maelezo, Dar es salaam
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji mstaafu Damian Lubuva ametoa
ufafanuzi juu ya ucheleweshaji wa matokeo ya awali ya ngazi Rais kutoka
majimbo mbalimbali nchini.
Akitangaza
matokeo hayo katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jana
jijini Dar es salaam Jaji Lubuva amesema kuwa Tume inasubiri matokeo
hayo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kutoka katika majimbo yote
nchini.
“waandishi
wa habari mnatakiwa kuwa wavumilivu na kutangaza kile ambacho
mnakisikia na si kupotosha umma kwani Tume inatoa matokeo bila
kupendelea chama chochote” aliongeza Jaji Lubuva.
Mbali
na hayo jumla ya majimbo 87 yameshaleta majibu ya awali ya matokeo ya
urais yakiwemo Mkoa wa Kusini Pemba Jimbo la Nchonga ambapo jumla ya
wananchi 8,018 walijiandikisha, 5949 walipiga kura na kura halali
zilikuwa 5771 ambayo ni asilimia 97.01 na 178.29 zilikataliwa.
Vilevile
katika Jimbo la Chunguni waliojiandikisha walikuwa 13,416 ambapo
wananchi 10,108 sawa na asilimia 75.34 walipiga kura, kura halali
zilikuwa 9,792 sawa na asilimia 96.92 pamoja na kura 311 zilikataliwa
ambayo ni sawa na asilimia 3.08.
Halikadhalika
katika Mkoa wa Mbeya Jimbo la Ileje jumla ya wananchi 56,002
walijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambapo asilimia
78.56 sawa na 43,997 walipiga kura, kati ya idadi hiyo kura 43,098
zilikuwa halali na kura 896 sawa na asalimia 2.04 zilikataliwa.
Jaji
Lubuva aliongeza kuwa katika Jimbo la Ileje mkoani Mbeya ACT ilipata
kura 501, ADC kura 347, CCM kura 26,368, CHADEMA kura 15, 651, CHAUMA
walipata kura 155, NRA kura 26,TLP kura 36, pamoja na kura 20 kutoka
chama cha UPDP.
Mbali
na hayo majimbo mengine yaliyowakilisha matokeo hayo ni pamoja an Jimbo
la Mtama kutoka Mkoa wa Lindi, Jimbo la Tunguu Mkoa wa kusini Unguja,
Jimbo la kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, Jimbo la Nachingwea, Jimbo la
mtama kutoka mkoani Lindi, Jimbo la Mafia mkoani Pwani pamoja Jimbo la
Mkuranga mkoani Pwani.
Pia
Mkoa wa Katavi Jimbo la Mpanda vijijini, Mkoa wa Magharibi Mjini Jimbo
la Fuoni, Jimbo la Kikwajuni, Jimbo la Mwera, Jimbo la Amani na Jimbo la
Magomeni Mkoa wa Unguja Jimbo la Nungwi, Kaskazini Unguja Jimbo la
Bumbwini, mkoa wa Rukwa Jimbo la nkasi kusini, Mkoa wa Kagera Jimbo la
Nkenge na Jimbo la Byalamuro, kutoka Mkoani Arusha Jimbo la Arusha
Mjini yaliwakilisha matokeo yao.
Kwa
upande wake Msaidizi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema Bwa. Matson
Chizi amesema kuwa mchakato mzima wa Uchaguzi ni mzuri wa wapo tayari
kupokea matokeo hayo kwa jinsi yatakavyokuwa.
No comments:
Post a Comment