Msimamizi wa Uchaguzi, Ali Kidwaka akitangaza matokeo ya Ubunge jimbo la Busanda na Geita.
Mbunge mteule wa Busanda Bi Lolesia Bukwimba akiongea na Wanahabari mara baaada ya kutangazwa mshindi.
Diwani Mteule wa kata ya Lwamgasa jimbo la Busanda, Joseph Kaparatus akishangilia ushindi baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
MBUNGE
mteule wa jimbo la Busanda wilayani Geita (CCM), Bi. Lolesia Jeremia
Bukwimba amesema kuwa atahakikisha ana shirikiana na wananchi wake
kutatua kero mbalimbali zinazo wakabili wanabusanda.
Bukwimba
amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi
baada ya msimamizi wa uchaguzi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
Geita,Ali Kidwaka kutangaza matokeo ya uchaguzi wa ubunge.
Amesema
kuwa kutokana ridhaa hiyo ambayo wananchi wa jimbo hilo wamempa
awatumikie tena ata hakikisha anatatua kero ya maji, afya, umeme na
miuondo mbinu ya barabara.
Awali
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Busanda Kidwaka alimtangaza Bukwimba
kuwa mbunge wa jimbo hilo baada kupata kura 63,043 sawa na asilimia
58, Ngofumani Batist Msafiri ACT wazalendo kura 1,532 sawa na
asilimia 1 Alphonce Mawazo chama cha Demokrasia na maendeleo
CHADEMA kura 45,019 sawa na asilimia 41.
Kidwaka
amesema kuwa wapiga kura walikuwa ni 68,041 na kura halali ni 64,850
idadi ya wapiga kura walikuwa wamejiandikisha ni 109,190 .
Katika
jimbo la Geita Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya hiyo, Ali
Kidwaka amemtangaza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa
Geita, Joseph Kasheku Msukuma kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada
ya kupata kura 44,313 sawa na asilimia 68% Severine Malugu CUF
kura 1,786 sawa na asilimia 3 Manglima Joseph Agustine (CHADEMA)
kura 18,909 sawa na asilimia 29
Wapiga kura walikuwa ni 68,041 kura halali ni 64.850 na waliokuwa wamejiandikisha kupiga kura ni 109,190 .
No comments:
Post a Comment