TAMKO LA ASASI ZA KIRAIA KUHUSU VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI WIKI MOJA KUELEKEA TAREHE YA UPIGAJI KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU TANZANIA TAREHE 25.10.2015
Asasi
za Tanzania tumeendelea kufuatilia mchakato wa uchaguzi mkuu 2015 tangu
uandikishaji wapiga kura, uhamasishaji hadi kampeni zinazoendelea kwa
umakini mkubwa.
AZAKI tumefanya hivyo tukiamini kuwa uchaguzi ni sehemu kuu ya michakato ya kidemokrasia hapa nchini kama ilivyo duniani kote. Sisi asasi za kiraia Tanzania, tukiwa watetezi na wasimamizi wa demokrasia, utawala bora na haki za binadamu, hatumuungi mkono mgombea yeyote wala chama chochote cha kisiasa kinachotafuta kuingia madarakani wala hatulengi kuchukua dola.

Kwa
ujumla wake, uchaguzi hufanikishwa na wadau wengi tukiwemo sisi AZAKI,
Vyombo vya usalama, viongozi wa Dini, Taasisi za Umma kama Tume na
Vyombo vya habari. Lakini makundi makuu mawili ya wahusika wakuu ni
wapiga kura na wapigiwa kura.
Ili wapiga kura waweze kuchagua kiongozi atakayeweza kusimamia maendeleo ya nchi na kuhakikisha amani ya nchi inazidi kudumu ni lazima viashiria vyote vya uvunjifu wa amani na mazingira ya vitisho kwa wapiga kura vijadiliwe na wadau na vidhibitiwe mapema.

Usalama
na amani wakati wote wa uchaguzi ni suala la muhimu sana na ndio maana
Asasi za Kiraia (AZAKI) nchini zimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 unakuwa wa kidemokrasia, wa haki na wa
amani.
Tanzania ni Taifa lenye amani kwa muda mrefu sasa, lakini tusipokuwa makini katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira ya haki na usawa huenda tukalitumbukiza taifa hili katika machafuko.
Angalizo hili ni muhimu zaidi kwa mwaka huu ambapo hamasa na mashindano vimekuwa kwa kiwango cha juu kuliko miaka mingine yoyote ya nyuma.

Ili
kuweza kuhakikisha uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 unafanyika kwa usalama
na amani AZAKI zimeona ni vyema kuanisha masuala mbalimbali yanayoweza
kupelekea uvunjifu wa amani nchini kama angalizo kwa sekta na taasisi
husika kuchukua hatua stahiki mapema.
Mchakato huu umejaa changamoto mbalimbali ambazo kama hakutakuwa na jitahada za ziada basi ni wazi kuwa tutakwenda kufanya uchaguzi tukiwa katika hali tete zaidi. Kati ya hizo changamoto nyingi zinazojitokeza, sisi wana AZAKI tumeanisha mambo sita makubwa yanayohitaji ufumbuzi wa haraka kabla ya tarehe 25 oktoba. Mambo hayo ni kama yafuatayo;

(i) Matumizi Makubwa ya nguvu ya Vyombo vya Usalama
AZAKI
zimegundua kuwa vyombo vya usalama kama Jeshi la Polisi na makundi
mengine ya usalama Tanzania Bara na Zanzibar zimekuwa zikilalamikiwa
sana kwa kuona kuwa tishio kwa wananchi badala ya kuwa msaada kwa
wananchi. Kwa mfano, majeshi haya yamekuwa yakifanya mazoezi waziwazi
na karibu na makazi ya watu suala linalopelekea kujenga uoga na hofu
kwa wananchi .
Pia baadhi yao wameonekana wakitapakaa kwenye makazi ya wananchi huku wakiwa wamevaa sare zao. AZAKI zinatambua umuhimu wa vyombo hivi kipindi cha uchaguzi, AZAKI tunataka vyombo hivi kufanya kazi zao bila kujenga hofu kwa wananchi na kwa mujibu wa Sheria.

Wito Wetu kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama
- Vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi zake kwa uweledi na tahadhari ya kutowatia hofu wananchi na wapiga kura. Vyombo vya ulinzi visitumie vitisho, nguvu, na silaha za kivita wakati wa mikutano ya kampeni na siku ya kupiga kura.
- Vyombo vya usalama kwa namna yoyote visiegemee upande wowote wa chama cha siasa bali vitende haki kwa vyama vyote na wananchi wote wakiwemo wagombea mmoja mmoja na wala visikubali kuyumbishwa na mamlaka yoyote nje ya sheria inayovipa mamlaka kutekeleza wajibu wao.
- Tunalishauri Jeshi la Wananchi wa Tanzania kutojihusisha na mchakato wa uchaguzi kuanzia kipindi cha maandalizi, cha kampeni, upigaji kura na baada ya upigaji kura.
(ii) Daftari la Wapiga Kura na Taarifa za Msingi
Kwa
mujibu wa Katiba na Sheria, Uchaguzi wa Tanzania unasimamiwa na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar( ZEC). AZAKI
zimebaini pia pamoja na kufanya vizuri katika hatua zingine Tume za
Uchaguzi kwa sasa zimeonyesha udhaifu mkubwa katika eneo la utoaji wa
taarifa za msingi kwa wadau na umma kwa ujumla.
Tumeshudia
ukinzani wa taarifa mbalimbali zinazotolewa na Tume kama taarifa za
idadi halisi ya wapiga kura walioandikishwa pamoja na idadi ya vituo vya
kupigia kura. Ukinzani wa takwimu za muhimu kama hizi ni jambo
linaloweza kupelekea uvunjifu wa amani kama lisipo simamiwa vyema.
Mambo haya pamoja na mengine yanawaweka wananchi katika hofu kubwa kwa kutokujua kama watapiga kura ama la na endapo idadi halisi ya wapiga kura ni ipi. Hofu inaongezwa na ukweli kuwa Sheria za uchaguzi Tanzania haziruhusu kulalamikia matokeo ya uchaguzi hususani katika ngazi ya urais.

Wito wetu kwa Tume za Uchaguzi
- Tume ya Taifa ya uchaguzi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar zitimize majukumu yao kisheria kwa kutangaza rasmi takwimu za mwisho za idadi ya vituo vya kupigia kura na kujibu hoja zinazaoibuliwa na wanasiasa badala ya kuwabeza na kuwapuuza.
- Tume Itoe Daftari la wapiga kura lenye vigezo vyote kwa wadau wote na wanachi kwa ujumla mapema iwezekanavyo ili kutoa fursa ya kurekebisha makosa yatakayobainika.
- Tume ibandike majina ya wapiga kura kwenye vituo vyote wiki moja kabla ya siku ya kupiga kura kama ilivyoahidi kwa ajili ya wapiga kura kujua vituo watakavyopigia kura.
- Tume za uchaguzi zifanye kazi kwa uhuru, kufuata sheria, kusimamia kanuni walizokubaliana na vyama vya siasa na kujiepusha kwa namna yoyote kukipendelea chama chochote wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.
- Tume zinapaswa kuhakikisha kuwa zimewapa mafunzo ya uhakika maofisa na wasidizi wa uchaguzi na kuchunguza mienendo yao kabla hawajawakabidhi vituo vya kazi ili kuepusha makosa yaliojitokeza wakati wa kuandikisha wapiga kura.
- Tume za Uchaguzi zinapaswa kufanya maandalizi mapema, pia kusambaza vitendea kazi vinavyotakiwa kwa wakati ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza siku ya upigaji kura pamoja na hisia kuwa baadhi ya maeneo yanacheleweshewa vifaa kwa makusudi.
- Tume zihakikishe kuwa watu wote wenye sifa na kustahili kupiga kura ambao hawakuandikishwa katika vituo waliko siku ya upigaji kura wanawezeshwa kufaidi haki yao ya kupiga kura kwa mujibu wa sheria.
- Tunazitaka Tume ziruhusu mawakala wa vyma vya siasa kuingia kwenye chumba cha mwisho cha ujumlishaji wa kura za urais (National Tallying Centre) ili kuondoa hofu ya kuibiwa kura. Ifamike kuwa matokeo ya urais yakishatangazwa hayawezi kupingwa mahakamani. Ni kinyume na taratibu za uchaguzi kuwazuia mawakala wa vyama vya siasa kuingia kwenye kituo kikuu cha kitaifa cha ujumlishaji wa kura.
- Tume zitangaze matokeo sahihi bila ya kuchelewesha ili kuepusha kutokea kwa vurugu zinazoweza kujitokeza.
(iii)Mgogoro wa Kusubiri Matokeo katika umbali usiopungua Mita 200
AZAKI
tumebaini kuwa jambo lingine linaloweza kuchangia uvunjifu wa amani ni
mgogoro uliobuka kuhusu uhuru wa wapiga kura kubaki vituoni katika
umbali usiopungua mita 200.
Kwa mujibu wa sheria ya Taifa ya Uchaguzi ya Mwaka 1985 sura ya 343 ya sheria za Tanzania kama zilivyopitiwa mwaka 2010 mpiga kura anapewa haki ya kupiga kura na kuondoka kuendelea na shughuli nyinginezo au kubaki kituoni kusubiri matokeo ili mradi anafanya hivyo katika umbali usiopungua mita 200 toka kituoni na kwamba hafanyi mkutano. Kwa tafsiri hii, mpiga kura hajalazimishwa kurudi nyumbani baada ya kupiga kura wala hajakatazwa kuwepo nje ya eneo la katazo la kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 104 (1).

Sheria
inamtaka mpiga kura asionekane ndani ya eneo la kituo cha kupiga kura
baada ya kumaliza kupiga kura(within the vicinity) na haimlazimishi
mwananchi arudi nyumbani mara baada ya kupiga kura au asogee umbali wa
mita 200 bali sheria ya uchaguzi inaweka bayana kwa wananchi/mpiga kura
kutokupiga kampeni au kuvaa nguo zenye alama au nembo ya chama chochote
katika siku hiyo.
Wito Wetu kwa Tume za Uchaguzi na Jeshi la Polisi
- Kwa kuwa hili limekuwa kawaida sasa katika chaguzi zilizopita hapa Tanzania wananchi kubaki vituoni na kusubiri matokeo karibu na vituo kwa umbali wa mita 200, na kutokana na ufinyu wa muda usioweza kutoa mwanya wa kurekebisha sheria hii, Tunazitaka Tume za uchaguzi zitumie busara katika kuamua suala hili kwa kupima faida na hasara za kuzuia wananchi kubaki vituoni kwa umbali wa mita 200 kama walivyozoea katika chaguzi zilizopita.
- Pia, Tume zitoe maelekezo yenye kuangalia zaidi maslahi ya Taifa kwa wananchi badala ya kusikiliza upande wowote kati ya wanaovutana kuhusu suala hili. Ushauri wetu kuhusu jambo hili ni kuwa wapiga Kura waamue kuendelea na shughuli zao baada ya kupiga kura lakini wanaotaka waweze kubaki vituoni kwa umbali wa mita 200 kwa kadri ya mapenzi yao huku wakiepuka kufanya kinachofanana na mikutano.
- Mahakama isadie kutatua mgogoro huu wa tafsiri ya kisheria ili kuepusha machafuko katika Taifa hili yanayoweza kutokana na imani kuwa kukatazwa kubaki vituoni kuna nia ya kutaka kufanya ujanja Fulani kuhusu kura zao ikiwemo kuziiba.
- Pia tunataka Jeshi la Polisi wasitumie nguvu yoyote kwa wananchi endapo itafika siku ya kupiga kura bila suala hili kupatiwa ufumbuzi. Hii ni kwa sababu kwa jinsi Sheria ilivyo, imeruhusiwa wananchi kubaki umbali wa mita 200 kutoka vituoni.
- Pia tunawataka wapiga kura endapo wataona umuhimu wa kukaa umbali wa mita 200 kusubiri matokeo, basi wafanye hivyo kwa unyenyekevu mkubwa ili kulinda amani na pia kuepuka kuzuia wananchi wengine kutumia haki zao.
(iv) Suala la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na watumishi waliohamishwa vituo vya kazi
Ni
kwa mara nyingine sasa katika uchaguzi mkuu wanafunzi wa vyuo vikuu
wanakoseshwa haki yao ya kupiga kura kwa sababu zisizoridhisha.
Wanafunzi wengi walijiandikisha katika maeneo ambayo hawatakuwepo siku ya kupiga kura na hawataweza kupiga kura zote tatu kutokana na kwamba vyuo vitakuwa vimefungwa siku hadi tarehe ya upigaji kura.
Aidha, baadhi ya watumishi wa umma waliohamishwa vituo vya kazi katika miezi na siku za karibuni nao wamejikuta katika hali ya ugumu waliyonayo wanafunzi na wanavyuo.

Wito Wetu kwa Tume za Uchaguzi
- Asasi za kiraia zinasisitiza watanzania walio katika makundi hayo mawili wapewe fursa ya kuwezeshwa kufanya taratibu za kisheria kuwawezesha kupiga kura ya Rais siku ya tarehe 25 Oktoba. Aidha, katika miaka ijayo, Tume zihakikishe kuwa technolojia ya habari inawezesha upigaji kuwa wa waliojiandikisha popote nchini bila matatizo yoyote kwa kuwa mfumo ni wa kielektroniki.
- Asasi za Kiraia hazioni ulazima wa Tamko la Tanzania Commission for Universities (TCU) kwamba vyuo vikuu visifunguliwe mpaka baada ya uchaguzi kwani amri hii inanyima wanafunzi wa vyuo hasa wale wachache walijiandikisha vyuoni haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kinaweza kuwa ni kichocheo cha uvunjifu wa amani. Suala hili linapaswa liangaliwe upya kwa miaka ijayo.
(v) Kauli za Vitisho na Lugha Chafu
Kwa
muda huu mchache uliobaki, vyama vya siasa na wanasiasa vinapaswa
kuendesha kampeni za kistaarabu zinazoheshimu misingi ya sheria na siasa
za ushindani ambazo zinatambua kuwa kuna kushinda na kushindwa.
Kwa hivyo, kusiwepo na kampeni za vitisho, matusi na ubaguzi wa aina yoyote na badala yake kuwepo kampeni za kistaarabu zinazoheshimu na zinazozingatia maadili ambayo vyama vyote vya siasa vimesaini ili kuliepusha Taifa hili na Machafuko.

Tunazitaka
Tume zote mbili kuchukua hatua haraka iwezekanavyo kwa wale watakaotoa
vitisho kwa wananchi ama kwa wagombea. Tumesikitishwa na kitendo cha
Tume kuacha kuchukulia hatua baadhi ya wanasiasa wanaotumia lugha za
vitisho kwa wananchi au vyama vinavyokiuka muda wa kumaliza kampeni za
uchaguzi.
Aidha,
tunavitaka vyombo vya habari vya umma kuacha mara moja kutoa fursa kwa
chama kimoja tu wakati tunafanya uchaguzi wa vyama vingi.
Taarifa za kila wiki za Baraza la Habari na Taarifa ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu zinaonyesha kuwa toka kampeni zianze vyombo vya Umma hasa TBC na Habari leo vimekuwa zikionesha wazi wazi kukipendelea zaidi chama Tawala katika habari zake na kuziacha ama kuzipa uzito mdogo taarifa za vyama vingine.

Tunakemea
na kuvitaka pia baadhi ya vyombo vya habari vya binafsi kuacha kutoa
taarifa za kichochezi na za uongo kwa wiki moja hii kuelekea siku ya
kupiga kura ili kulinda amani ya Taifa.
Kipekee, tunapenda kuvipongeza vyombo vya habari ambavyo vimefuatilia na kutoa taarifa za kampeni za uchaguzi wa Tanzania 2015 kwa uhuru na haki wakati wote wa mchakato huu.
Kwetu, tunaona kuwa vyombo hivyo vimechangia kudumisha amani na vinastahili tuzo maalum.

Pia
kwa umoja wetu tunatoa tahadhari kwa AZAKI na viongozi wake
kutokushiriki katika shughulizi za kampeni za vyma na wagombea ili
waweze kutimiza wajibu wa uwaanngalizi bila kukiuka maadili ya AZAKI.
Tunawasihi
viongozi Wakuu wa Kitaifa wastaafu hasa Marais kutokuonyesha upande
kipindi cha uchaguzi na nyakati zingine zote ili waweze kuwa wasuluishi
endapo hali ya amani na usalama itapotea.
Taifa linahitaji wasuluhishi wa ndani hivyo ni vyema viongozi wakuu wastaafu wakalizingatia hili ukizingatia Tanzania tumekuwa tukisifika kwa kuwa wasuluishi wa majirani zetu.
Taifa linahitaji wasuluhishi wa ndani hivyo ni vyema viongozi wakuu wastaafu wakalizingatia hili ukizingatia Tanzania tumekuwa tukisifika kwa kuwa wasuluishi wa majirani zetu.
Mwisho
Sisi
ni Asasi za Kiraia (AZAKI) za nchini Tanzania zilizoundwa na
kutambulika kisheria na zinazofanya kazi katika masuala mbalimbali ya
kisheria, kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
Kwa umoja wetu tunasimamia na kuhimiza utawala wa sheria na haki za binadamu na masuala yote ya kimaendeleo ili kuhakikisha maisha ya watanzania yanakuwa bora katika nyanja zote.
Kwa sababu hiyo, tunajiona tukiwa na jukumu kubwa la kukemea na kuvitaka vyombo husika kufanyia kazi viashiria vyote vya uvunjifu wa amani ili kulinusuru Taifa letu. Kamwe hatuwezi kunyamazia uovu wala kunyamazishwa!

Imetolewa
kwa niaba ya AZAKI 300 nchini na asasi miavuli zilizofanya mikutano
mikuu ya mashirika wanachama kati ya tarehe 14 na 17 Oktoba 2015,
Dar es Salaam
Tarehe 17/10/2015 na:
Ismail Suleiman
Katibu Mkuu
Baraza la Taifa la Asasi za Kiraia
No comments:
Post a Comment