Nyumba ya makazi ya mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia imeteketea kwa moto siku ya Jumamosi, majira ya saa saba u nusu mchana, kwa kile kilichoelezwa kuwa huenda ni hitilafu ya umeme unaosemekana kukatika asubuhi na kurejea mchana kwa nguvu kubwa.
Akizungumza
na Channel TEN, kaka wa Mbatia, Felix Kessy amesema hadi sasa
wanachoweza kueleza ni uharibifu uliotokea kutokana na moto huo, kwani
hawakuwepo wakati wa tukio, ingawa anawashukuru majirani walioweza
kuokoa baadhi ya vitu vya ndani.
Amesema ni mapema mno
kuzungumzia aina ya uharibifu kwani atakayeweza kujua zaidi ni mkewe na
Mbatia ambaye kwa wakati huo Channel TEN ilipofika, haikuweza kuzungumza
naye kwa sababu alikuwa amepandwa na shinikizo la damu kutokana na
tukio hilo.
Mkuu wa oparesheni hiyo kutoka kikosi cha zima moto
na uokoaji kwa wakati huo nyumbani hapo sajenti Haji Madulika amesema
kikosi chake kiliwahi eneo la tukio ingawa kutokana na ukubwa wa moto,
walishindwa kuokoa baadhi ya vitu.
Aidha ameoneshwa kushangazwa kwake na tabia ya watu kuwashutumu askari wa zimamoto kwa kuchelewa huku wananchi wakielewa hali halisi ya barabara na miundombinu.
Aidha ameoneshwa kushangazwa kwake na tabia ya watu kuwashutumu askari wa zimamoto kwa kuchelewa huku wananchi wakielewa hali halisi ya barabara na miundombinu.
No comments:
Post a Comment