Mchoraji wa miundo
ya magari nchini India Sudhakr Yadav amejaribu kuweka rekodi ya pili ya
Guiness kwa kutengeneza gari analotumai litakuwa ndilo kubwa zaidi
duniani.
Gari hilo, ambalo limeundwa likifanana na gari aina ya
Ford Toure lililoundwa mwaka 1922, lina urefu wa futi 26 (mita 8) kwenda
juu na ukubwa wa futi 50 lina ukubwa maradufu wa basi lililo na ghorofa
mbili mjini London.Bwana Yadav tayari anashikilia rekodi ya kitabu cha Guiness kwa kuwa na baiskeli ndefu zaidi duniani.
Mchoraji huyo wa miundo ya magari anamiliki makavazi ya magari katika mji wa Hyderabad ulioko kusini mwa India ambapo anaonyesha mitindo tofauti ya magari.
Magari hayo yana maumbo na ukubwa tofauti .
''Tunalenga kuvunja rekodi ya kitabu cha Guiness kwa kuunda gari kubwa duniani. Ni rekodi mpya na nina matumaini nitaipata," alisema.
Anatarajia gari hilo liwe na mngurumo sawa na wa magari ya mbio za langalanga au Formula One.
Baiskeli yake ya magurudumu matatu ni ndefu zaidi ya gari hilo ikiwa na futi 41.5 kwenda juu.
No comments:
Post a Comment