Mwenyekiti
wa Mtandao wa Kimataifa wa Wabunge (PGA) Mhe. Pindi Chana ( MB)
akimkabidhi Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa, Bw.Mogens
Lykketoft,Tamko la wabunge lenye sahihi 607 za wabunge kutoka mataifa 70
la kutokomeza ndo za utotoni na za kulazimisha katika hafla fupi
iliyofanyika Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu
Mwakilishi
wa Kudumu wa Zambia katika Umoja wa Mataifa, Balozi Dr. Mwaba
Kasese-Bota akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo alianisha mipango
mbalimbali inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
wakiwamo viongozi wa kimila katika kuzunguia ndoa za utotoni na za
kulazimishwa.
Mwakilishi
wa Kudumu wa Ghana katika Umoja wa Mataifa, Balozi Martha Anna Akyaa
Pobea naye akitoa mchango wa namna gani serikali yake
inavyolishughulikiwa tatizo za ndoa za utotoni ambapo amesema katika
nchi za Afrika Magharibi katika kila watoto watano wa kike, wawili
huolewa kabla ya kutimiza miaka 18 na kwamba ndoa hizo za utotoni si tu
kwamba zinadumaza ukuaji wake lakini pia zinachaniga mimba za umri
mdogo, vifo vitokanavyo na uzazi, maambukizi ya magonjwa mbalimbali na
kuchangia umaskini kwa watoto wengi wa kike.
Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo wakiwamo watalamu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu, Bi, Nuru Milao
Na Mwandishi Maalum, New York
Mtandao wa Kimataifa wa Wabunge kutoka Mabunge mbalimbali Duniani (PGA), umemkabidhi Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa Bw. Mogens Lykketoft, tamko la kukomesha ndoa za utotoni na za kulazimishwa kwa watoto wa kike.Akikabidhi tamko hilo lenye sahini Zaidi ya 607 kutoka nchi 70 Mwenyekiti wa Mtandao huo wa wabunge, Mhe. Pindi Chana na ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto amesema, kukabidhiwa kwa tamko hilo kwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kunakwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike ambayo huadhamishwa kila Octoba ya mwaka.
Mtandao wa Kimataifa wa Wabunge kutoka Mabunge mbalimbali Duniani (PGA), umemkabidhi Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa Bw. Mogens Lykketoft, tamko la kukomesha ndoa za utotoni na za kulazimishwa kwa watoto wa kike.Akikabidhi tamko hilo lenye sahini Zaidi ya 607 kutoka nchi 70 Mwenyekiti wa Mtandao huo wa wabunge, Mhe. Pindi Chana na ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto amesema, kukabidhiwa kwa tamko hilo kwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kunakwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike ambayo huadhamishwa kila Octoba ya mwaka.
Mwenyekiti
wa PGA, amesema wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika hapa Umoja wa
Mataifa, siku ya Jumatatu kwamba, ushirikiano wa wadau mbalimbali hasa
wabunge , serikali na asasi za kiraia ni muhimu sana ikiwa jumuiya ya
kimataifa inataka kuondokana na kumaliza tatizo la ndoa za utotoni na
za kulazimishwa.
Mhe.
Pindi Chana, amesema, ni kwa kutambua ukweli huo ndiko kulikopelekea
kuanzishwa kwa mtandao huo mwezi Machi mwaka huu ambao moja na dhumuni
lake kubwa ni kuwahamasisha, kuwaelimisha na kuwawezesha wabunge kutumia
nafasi zao kukemea tatizo hilo.
Hafla
hiyo iliandaliwa kwa ubia kati ya Wakilishi za Kudumu za Tanzania,
Zambia , Ghana na Canada katika Umoja wa Mataifa. nchi ambazo kwa
namna moona ama nyingine zimekuwa mstari wa mbele katika kuchangiza
afya na maendeleo ya mtoto wa kike ili mtoto huyo wa kike aweze kupata
fursa kukua, kuelimika na hatimaye aweze kulitumikia taifa lake na
watu wake katika ukamilifu wake.
Amebainisha
kwamba kama viongozi, wabunge wanapashwa kuwahabarisha wananchi wao,
na wabunge wenzo thamani ya mtoto wa kike, na umuhimu wa kuhakikisha
kuwa mtoto wa kike anakwenda shule, anabaki shule na anamaliza masomo
yake.
“
Kama watunga sheria, wabunge tunapaswa kusimamia sheria zinazomlida
mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na kupitisha sheria zitakazo ainisha
bayana umri wa kuolewa kwa mtoto wa kike ambao unapashwa kuwa miaka kumi
na nane” amesititiza Mwenyekiti wa PGA.
Aidha
Mhe.Pinda Chana akaongeza pia kuwa wabunge na mabunge yanao wajibu wa
kusimamia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, na ugawaji wa
raslimali kwenye maeneo mpaya ya kisera na sera ambazo tayari zipo.
Akaongeza kuwa Lengo namba 5.3 la maendeleo endelevu linaainisha wazi
wazi namna ya kushughulikia vitendo vinavyorudisha nyuma maendeleo na
ustawi wa mtoto wa kike katika kile eneo, jambo analosema wabunge
wanapashwa kusimamia vema utekelezi wa lengo hilo pamoja na mengine.
PAG
inalenga pia kuwaelimisha wabunge kutetea na kusimamia haki
zinazomlinda mtoto wa kike, kupiga vita mila na desturi potofu
zinazomkandamizi mtoto wa kike , kusimamia utawala wa sheria, demokrasia
usawa wa binadamu, kupinga ubaguzi na kusimamia usawa wa kijinsia.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa tamko hilo, Rais wa Baraza Kuu la 70 la
Umoja wa Mataifa, Bw. Lykketoft amesema kuwa tamko hilo limekuja wakati
muafaka na hasa baada ya Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali
kupitisha kwa kauli moja Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu (
Agenda2030) mwezi uliopita.
Akaongeza
kuwa, akiwa Rais wa Baraza Kuu la 70 atahakikisha kwamba nchi
wanachama wa Umoja wa Mataifa zinaendelea na majadiliano yenye tija na
yakayolenga katika kuhakikisha utekelezaji wa Agenda 2030 na kutilia
mkazo mijadala inayolenga katika mkomboa mtoto wa kike dhidi ya ndoa
za utotoni na za kulazimishwa. Na pia kuhakisha kwamba majadiliano
kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yanafanyika kwa lengo la siyo tu
kuiokoa sayari dunia lakini pia maisha ya mwanadamu ambayo uhai wake
unategemea sana uwepo wa sayari hiyo.
No comments:
Post a Comment