Mgombea urais kupitia chama cha TLP Macmillan Lyimo amesema anaunga mkono kauli ya mwenyekiti wake wa chama Mh. Augustine Mrema ya ‘kumpigia debe’ mgombea wa chama cha mapinduzi CCM, Dk John Magufuli, kwa madai kuwa hayo ni maamuzi yake binafsi.
Akizungumza
na East Africa Radio mchana huu, Lyimo amesema kuwa kauli hiyo
haijatolewa na mkutano wowote wa chama, bali ni maoni binafsi kwa kuwa
mwaka huu watanzania wanachagua mtu na siyo chama na kwamba jambo
alilofanya Mrema si jipya wa la ajabu.
“Hili
jambo siyo la ajabu, hata Marekani, Colin Powell alitangaza kumuunga
mkono Obama licha ya kuwa chama tofauti, Mrema amesema hivyo kwa kuwa
anajua looser siyo yeye, tumesimamisha wagombea ubunge nchi nzima, na
yeye ni mmoja wapo, kwahiyo hilo halinipi shida” Amesema Macmillan Lyimo
Kuhusu
mahusiano kati yake na mwenyekiti huyo, Lyimo amesema kuwa mahusiano
ndani ya chama hicho ni mazuri na hakuna ugomvi wowote.
“Tunaendelea kushirikiana kama kawaida, na hata kampeni zangu nilianzia kwake na nitafungia jimboni kwake” kauli ya Lyimo
Kuhusu nafasi yake ya ushindi, Lyimo amesisitiza kuwa yeye ndiye atakayeshinda urais mwaka huu, na kamwe Rais hatoki CCM
“Magufuli
hawezi kushinda, nafasi kubwa ya ushindi ninayo mimi, hata Magufuli
anajua kuwa mimi napinga huo mwenge kwenye picha yake, hiyo ni ishara ya
uchawi, na uchawi wake utashindwa mwaka huu”. Amesema mgombea huyo
No comments:
Post a Comment