Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ulanga, kimemchagua mtoto wa kwanza wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani, Godluck Mtinga kuwania ubunge katika Jimbo la Ulanga Mashariki.
Katibu
wa CCM wa wilaya hiyo, Mathias Mbogo alisema Mtinga (pichani) aliibuka
kidedea kwa kupata kura 731 kati ya 1,029 zilizopigwa na kupendekezwa
kuwania nafasi hiyo iliyokuwa inawaniwa na mama yake aliyefariki dunia
Septemba 24, mwaka huu nchini India.
Alisema
idadi ya wapigakura waliojitokeza walikuwa 1,029, lakini kura halali
zilikuwa 1,025 huku nne zikiharibika. Aliwataja wagombea wengine katika
uchaguzi huo kuwa ni Aziz Aziz aliyepata kura 134, Omari Dokodogo kura
52, Augustino aliyepata kura 41, Wenslaus Mkunla kura 39, Faustine Kipau
11, Herieth Mwakifulefule tisa na Daud Kitolelo aliyepata kura nane.
Kwa
mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), uchaguzi wa majimbo ya
Ulanga Mashariki na Lushoto ulioahirishwa kutokana na vifo vya wagombea
utafanyika Novemba 22, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment