Dr.
Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa
serikali (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Magavana
wa Mashariki na Kusini mwa Afrika baada ya mkutano wa MEFMI.(Picha na
Eva Valerian, Peru – Lima).
Katika
kipindi hiki cha mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la
Fedha la Kimataifa, kumekuwa na mikutano mbalimbali inaendelea hapa
nchini Peru. Mikutano hiyo inaendeshwa na Taasisi mbalimbali zenye
utaalamu wa kiuchumi na kifedha. Akizungumza na waandishi wa habari,
katibu Mkuu Wizara ya fedha Dr. Servacius Likwelile alisema “MEFMI ni
chombo kikubwa kwa Afrika Mashariki na Kusini katika kutoa mafunzo ya
usimamizi wa mambo ya uchumi kwa watendaji wa nchi wanachama.”
Aliendelea kusema kuwa katika siku hizi mbili wamekutana na chombo hicho
kwa madhumuni ya kuzungumzia maendeleo ambayo yanatokana na rasilimali
kama vile gesi na madinii na kutoa mapendekezo ya namna gani Afrika
inaweza kusimamia rasilimali hizo.
Akitoa
ufafanuzi katika majadiliano hayo Dr. Likwelile alisema”Tanzania kuna
rasilimali nyingi kama vile gesi ambayo imegunduliwa Mtwara na
kusisitiza kuwa kuna nchi mbalimbali barani Afrika ambazo zina dhahabu
ya kutosha ambayo inaweza kuinua uchumi wa Afrika kama kutakuwa na
utaratibu mzuri wa kuzitumia.
“Lengo
kuu la mkutano wa MEMFI ni kuzungumzia shughuli zinazofanywa na MEMFI
ili kuwezesha kupanga namna ya kuboresha uwezo na kuendesha shughuli
zetu katika kuinua uchumi wa Afrika kwani tutahitaji fedha nyingi kwa
ajili ya kuwekeza kwenye miundombinu lakini lazima tuhakikishe kwamba
tunafanya hivyo ili kuhakikisha uchumi wetu unakuwa imara na kunakuwa
na utaratibu wa kuweka akiba kwa ajili ya vizazi vijavyo, hili ni suala
la msingi sana” alisistiza Likwelile.
Likwelile
aliongeza kuwa “Vizazi vingi vinatumia rasilimali zote bila kuangalia
utaratibu wawakati ujao kuwa utakuwaje, hivyo katika kikao hiki
tumekubaliana kuanzisha mfuko ambo ni kwa ajili ya kuwekeza kwa ajili ya
matumizi ya baadae (Sovereign Wealth Fund). Masharti ya mfuko
huoyatakuwa ni kama ifuatavyo: (i) Mfuko huo lazima uweze kuzalisha
ajira, (ii)Mfuko huo lazima uwe na misingi imara ya kusimamia uendeshaji
wa shughuli zake,(iii) Mfuko lazima uwe na chombo imara kinacho
kisimamia mfuko huo. (iv) Lazima kuwe na utaratibu ambao unasema mfuko
huu utafanya nini na hautafanya nini.
La
msingi kuwe na mfumo wa kisheria lakini tuangalie rasilimali watu ili
kuweza kuhifadhi mfuko huo. Na namna gani miundombinu itawezakusaidia
kuimarisha uchumi ili uweze kutambuliwa.”
Naye
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu alisema kuwa,ni
muhimu kujua mapato yetu yatokanayo na upatikanaji wa madini kwani
tunaweza kuyatumia vizuri katika kuhakikisha tunatengeneza miundombinu,
kuongeza uwezo wa kuzalisha na baada ya hapo nchi iweze kuendelea kupiga
hatua hata kama madini yatakuwa yamekwisha.
Waziri
wa Fedha ni Gavana katika mikutano hii, akifuatiwa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile
ambaye ni Gavana msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia (WB), aidha
Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa
Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Hali ya hewa mjini hapa ni baridi, rasharasha na manyunyu ya hapa na pale hasa nyakati za asubuhi.