Mwenyekiti
wa Antibiotic Resistance Partnership (GARP), Profesa Said Aboud kutoka
Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba Shirikishi (MUHAS) kushoto akitoa ripoti
ripoti ya dunia kuhusu matumizi na usugu wa dawa za Antibiotiki ya mwaka
2015,uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii.Katikati ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakarina
kulia ni Mfamasia Mkuu wa Serikali Henry Irunde.
Mganga
Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari (kushoto wa pili) akizindua
ripoti ya dunia kuhusu matumizi na usugu wa dawa za Antibiotiki ya mwaka
2015,uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii. Kushoto ni Mwenyekiti wa Antibiotic Resistance Partnership
(GARP), Profesa Said Aboud kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba
Shirikishi (MUHAS)na kulia wa pili ni Makumu Mwenyekiti wa wa Antibiotic
Resistance Partnership (GARP), Profesa Robinson Mdegela kutoka Chuo
Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na kulia wa pili ni Mfamasia Mkuu wa
Serikali Henry Irunde.
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari akionesha ripoti hiyo.
Picha ya pamoja kati ya Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari na wadau wa uzinduzi huo.
Na Magreth Kinabo – Maelezo
Juhudi
zaidi zinahitajika na utashi wa kisiasa katika kudhibiti usugu wa
dawa za antibiotiki ili isije ikafikia mahali ambapo dawa hizo
zikakosekana katika kutibu magonjwa ya kuambukiza, pia wito umetolewa
kwa jamii kuwa na matumizi sahihi ya dawa za antibiotiki ili kuweza
kupunguza usugu wa dawa hizo.
Hayo
yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Antibiotic Resistance Partnership
(GARP), Profesa Said Aboud kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba
Shirikishi( MUHAS) wakati wa uzinduzi wa ripoti ya dunia kuhusu matumizi
na usugu wa dawa za Antibiotikiya mwaka 2015,uliofanyika kwenye ukumbi
wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambapo alisema ripoti
hiyo imetoa mapendekezo hayo.
Aidha
tatizo la usugu wa dawa hizo linachangiwa na kutokuwepo kwa usimamizi
madhubuti katika kununua dawa kutoka katika maduka ya dawa bila cheti
cha daktari.
Akizungumzia
kuhusu suala hilo, Profesa Aboud alisema Watafiti wa Kituo cha
Kimataifa cha Utafiti wa Magonjwa, Uchumi, na Sera(Center for Disease
Dynamics,Economics & Policy(CDDEP) )wakishirikiana na nchi washiriki
ikiwemo Tanzania walitoa ripoti mpya inayoonesha kiwango kikubwa cha
usugu wa dawa hizo zinazotumika kutibu magonjwanya kuambukiza ambayo
yanapelekea kuhatarisha maisha ya watu dunia.
Alisema
ripotoi hiyo ilizinduliwa Septemba 17,mwaka 2015 mjini
Washington,Marekani inaonyesha usugu na matumizi yasiyosahihi ya dawa za
antibiotiki na mipango ya kitaifa inayotumika katika kupambana na
tatizo hilo.
“The
State of the World’s Antibiotics 2015 ni ripoti ya kwanza kuonyesha kwa
kina ukubwa wa tatizo la usugu wa dawa za antibiotiki kidunia kwa
binadamu, wanyama na mazingira. Ripoti hiyo imetoa mikakati mipya ambayo
kila nchi ikiwemo Tanzania ionapendekezwa kuifanyia kazi ya kupambana
na tatizo hilo linaloenea kwa kwa kasi.
“Ripoti
hiyo inaonyesha kuwa matumizi sahihi ya dawa za antibiotiki kutibu
magonjwa ya kuambukiza ni mojawapo ya njia muhimu kupambana na usugu wa
dawa za antibiotiki na hili likiwezekana litaondosha dhana kuwea
suluhisho la usugu wa dawa za antibiotiki ni kukosekana kwa dawa mpya za
antibiotiki za kutibu magonjwa ya kuambukiza ,” alisema Profesa Aboud.
Aliongeza
kwamba nchi tajiri duniani zinatumia dawa za antibiotiki kwa kiasi
kikubwa ,tatizo la usugu wa dawa za antibiotiki kwa nchi masikini na
zenye uchumi wa kati ni kubwa duniani linahitaji juhudi za makusudi
kupambana nalo.
Profesa
Aboud alisema tafiti zilizofanyika Tanzania zinaoyesha kuwa kuna
kiwango kikubwa cha usugu kwa dawa za antibiotiki kwa bakteria aina ya
Streptococcus pneumonia anayesababisha homa ya mapafu kwa watoto.
Magonjwa ya kifua pamoja na homa ya mapafu yanasababisha kwa asilimia 15
ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano katika mwaka 2013 na
Watanzania 35,000 walikufa kwa homa ya mapafu mwaka 2012 kutokana na
bacteria sugu aina ya Streptococcus pneumonia.
Alifafanua
kwamba usugu wa dawa hizo umeonekana katika vinyememea vya maradhi vya
bacteria katika uambukizo wa njia ya mkojo,kisonono na kaswende katika
miaka 15 iliyopita.
“
Kama hali ya usugu wa dawa za antibiotiki itaachwa kuendelea ,magonjwa
Ya kisonono na kaswende hayatatibika na kusababisha ugumba na upofu wa
watoto wa change wanaozaliwa,” alisisitiza.
Alisema
kwa mara ya kwanza ripoti hiyo inaonyesha taarifa kutoka nchi masikini
kama Tanzania na zenye uchumi wa kati ambapo tatizo la usugu wa dawa za
antibiotiki ni kubwa lakini haionyeshi juhudi za makusudi zikichukuliwa
kupambana na tatizo hilo.
Ripoti
hiyo imetumia uzoefu uliopatikana kutoka nchi nane katika Afrika
ikiwemo Tanzania na Asia kupitia mradi wake wa kimataifa wa kupambana na
usgu wa dawa za antibiotiki(Global Antibiotiki Resistance
Partnership(GARP).
Alizitaja
njia nyingine ambazo zimetolewa kama mapendekezo yanayowezakutumika
kupambana na tatizo hilo kuwa ni kuwa na kampeni ya matumizi sahihi ya
dawa hizo kutibu magonjwa ya kuambukiza, kudhibiti magonjwa ya
kuambukiza katika hospitali, kutoa chanjo kukinga magonjwa ya
kuambukiza na kupunguza matumizi ya antibiotiki yasiyo ya lazima ya
lazima kutibu magonjwa ya kuambukiza, ikiwemo na utoaji wa elimu kwa
umma.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari alisema
Serikali imeyapokea mapendekezo ya ripoti hiyo, hivyo wizara yake itatoa
miongozo juu ya suala hilo baada ya kujadiliana na wataalamu
mbalimbali.