Tume ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza James Mbatia wa NCCR
Mageuzi kuwa mbunge mteule wa jimbo la Vunjo huku kada wa Chadema,
Anthony Komu naye akiibuka mshindi katika jimbo la Moshi Vijijini
lililokuwa linaongozwa na Waziri wa zamani wa Biashara na Viwanda, Dk.
Cyril Chami kupitia CCM.
Akitangaza matokeo ya majimbo
hayo mawili mkoani Kilimanjaro kuamkia leo, msimamizi Fulgence Mponji,
amesema Mbatia amepata kura 60,187 akiwashinda wapinzani wake; Innocent
Shirima wa CCM aliyepata kura 16,617 na Augustine Mrema wa TLP aliyepata
kura 6,416.
Kutokana na matokeo hayo, Mrema
ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Vunjo huku
wananchi wa eneo hilo wakiendeleza historia ya kutomchagua mbunge wa
chama kimoja kwa vipindi viwili tangu kurudi kwa mfumo wa siasa za vyama
vingi.
Kwa upande mwingine, CCM imepoteza jimbo la
Moshi Vijijini kupitia kwa mgombea Cyril Chami na kurudi tena upinzani
baada ya kada wa Chadema, Anthony Komu kutangazwa mshindi. Hata hivyo,
waziri huyo wa zamani wa Viwanda na Biashara hakuwepo wakati NEC wa
kusaini kuonyesha kuwa amekubali matokeo.
Kwa mujibu wa
Mponji, mbunge mteule wa Moshi Vijijini, Komu amepata kura 55,813 huku
Dk Cyril Chami akijikusanyia kura kura 24,415.
No comments:
Post a Comment