Kupitia
taarifa hii kwa vyombo vya habari, tunapenda kuutaarifu umma wa
Watanzania wote nchini kuwa Mgombea Urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na
vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Mh. Edward
Ngoyai Lowassa atahutubia taifa kupitia vituo mbalimbali vya
televisheni, redio na njia zingine za upashanaji habari hususan mitandao
ya kijamii (live streaming facebook, twitter, forums etc), siku ya
Ijumaa, tarehe 23 Oktoba, 2015, saa 3 usiku.
Kupitia
hotuba hiyo kwa taifa, Mh. Lowassa atazungumza na Watanzania wote,
ndani na nje ya nchi, na watu wa mataifa yote, kuhusu Tanzania mpya
itakayotokana na MABADILIKO makubwa ya kimfumo, kiutawala na utendaji wa
serikali atakayoiunda baada ya Watanzania kumpatia dhamana ya kuwa Mkuu
wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu na Kiongozi Mkuu wa Serikali hapo Oktoba 25,
2015.
Aidha,
Mhe. Lowassa atatumia muda huo kuwashukuru Watanzania wote kwa namna
walivyomuunga mkono kwa upendo mkubwa yeye, mgombea mwenza wake, Juma
Duni Haji, chama na UKAWA kwa ujumla katika uchaguzi huu wa MABADILIKO,
ya kuhitimisha utawala wa nusu karne wa CCM kuliandaa taifa na uongozi
mpya utakaotoa utumishi wa kuliondoa taifa hapa lilipokwama katika
umaskini, ujinga, maradhi na ufisadi unaowatafuna Watanzania.
Hiyo ni dalili ya wazi kwamba serikali atakayoiunda itatokana na watu kwa ajili ya watu ambao ni umma wa Watanzania wote.
Imetolewa Alhamis, Oktoba 22, 2015 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment